26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waliokaidi kulipia kodi ya ardhi Mara kufikishwa Mahakamani

Na Shomari Binda,Musoma

IDARA ya Atdhi mkoa wa Mara,imesema katika kipindi hiki Cha mwezi januari 2021 itaanza kutafikisha Mahakamani wananchi waliokaidi kulipia kodi ya ardhi kwa mwaka 2019/2020.

Akizungumza na MtanzaniaDigital ofisini kwake, Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Mara, Jerome Kiwia amesema muda uliotolewa na unaotakuwa kulipia kwa mujibu wa sheria umemaluzuka na sasa taratibu nyingine zinaendelea.

Amesema idara ya ardhi mkoa wa Mara imekuwa ikitoa taarifa kila wakati juu ya kulipa kodi na umuhimu wa kodi hiyo lakini wapo ambao bado wamekaidi na hatua inayofuata ni kufikishwa Mahakamani.

Kiwia amesema katika kipindi cha Oktoba na Novemba baada ya utoaji wa taarifa wapo waliojitokeza kulipia kodi ya ardhi ya maeneo yao.  

Amesema kodi ya ardhi ya kipindi cha mwaka 2019/2020 inapaswa kulipwa Juni 2020 na kutolewa muda hadi Desemba 31, lakini wapo ambao hawajalipia kodi hiyo.

“Tumekuwa tukitoa taarifa mara kwa mara ya kuwataka wananchi kulipia kodi ya ardhi kwa mujibu wa sheria kwenye maeneo wanayoyamiliki, muda uliotolewa wa kulipia umemalizika na sasa unaandaliwa utaratibu wa wadaiwa wote kufikishwa Mahakamani na kuweza kupatikana kodi ya serikali,”amesema Kisia.

Kamishna huyo Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Mara, amewataka wananchi wote wa maeneo yaliyopimwa lakini hawana hati kufika kwenye ofisi za watendaji wa Kata na serikali za mitaa kuchukua fomu kwaajili ya kulipia maeneo yao.

Amesema kwa mujibu wa sheria wananchi wanaomiliki ardhi hata kama hawana hati wanapaswa kulipia na utaratibu wa kupata hati ni kwa muda wa wiki moja baada ya kukamilishwa kwa taratibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles