28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kamonga ashauri lesini za madini 201 kufutwa

Na Mwandishi Wetu, Njombe.

Mbunge wa Ludewa Mkoani Njombe, Wakili Joseph Kamonga, ameshauri serikali kufuta leseni 201 za wamiliki wa vitalu vya madini wilayani Ludewa ambao hawafanyii kazi maeneo hayo ili kutoa nafasi kwa wachimbaji wadogo wenye uwezo wa kuyaendeleza.

Ushauri huo aliutoa mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Njombe (RCC), baada ya kupata taarifa kutoka kwa kaimu ya afisa madini, Mhandisi Fredrick Jirenga ambapo alisema kuwa wilaya ya Ludewa ina jumla ya leseni 201 za umiliki wa maeneo ya madini lakini kati ya hizo zinazofanya kazi ni tano pekee.

“Naishukuru ofisi ya madini Mkoa wa Njombe kwa kuweka data hizi hadharani,zamani haikua hivi tumeambiwa wilaya ya Ludewa zipo leseni za madini 201 lakini zinazo fanya kazi ni tano pekee, nashauri leseni hizi zifutwe bila kujali mmiliki ni nani ili kutoa nafasi kwa wachimbaji wadogo wenye uwezo wa kuyafanyia kazi maeneo hayo,”alisema Kamonga.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere, alisema kuna maeneo yapo nje ya miradi ya Liganga na mchuchuma Wilayani humo ambayo yalipaswa kumilikiwa na Wachimbaji wadogo lakini yamechukuliwa na NDC na kuwanyima Fursa Wachimbaji hao jambo ambalo linapaswa kutazamwa ili NDC wayaachie na kutoa fursa kwa wachimbaji wadogo.

“Katika miradi ya chuma na makaa ya mawe wilayani ludewa kuna maeneo yapo nje ya mradi hii lakini yapo chini ya NDC, Ombi langu hawa NDC wayaachie ili wapewe wachimbaji wadogo ambao wanauhitaji wa kufanya kazi na kutoa fursa kwao na serikali,”alisema Tsere.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya, alisema serikali inaendelea kupitia mkataba wake na mwekezaji ambao ulikua unampa faida zaidi mwekezaji kwa asilimia 80 huku serikali ikibaki na asilimia 20 pekee na kwamba ofisi yake itawasilisha ombi kwa Rais Dk John Magufuli la kuanza kuifanyia kazi miradi hiyo.

Pia alisema kuwa ofisi yake itazungumza na Shirika la Maendeleo nchini NDC liwaachie wachimbaji wadogo baadhi ya maeneo yaliyopo nje na miradi ya chuma na makaa ya mawe wilayani Ludewa waweze kufanyia kazi huku akibariki uamuzi wa kuzifuta leseni ambazo kwa muda mrefu hazifanyi kazi na kuishia kumiliki maeneo bila faida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles