26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Desk and Chair waunga mkono kampeni ya nyumba ni choo

Na Sheila  Katikula, Mwanza

Taasisi ya Desk Chair Foundation ya jijini Mwanza imeunga mkono kampeni ya Nyumba  ni Choo kwa kujitolea kujenga vyoo 20 yenye thamani ya Sh milioni  50 kwenye shule ya sekondari ya kilole ili kuwakinga wanafunzi na magonjwa ya mlipuko.

Msaada huo unakuja baada ya  wanafunzi wa kike kutambua upungufu huo na kupeleka maombi kwenye taasisi hiyo ili iweze kuwasaida kukabiliana na tatizo la upungufu wa matundu ya vyoo shuleni hapo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Ofisini kwake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sibtain Meghjee alisema walipokea barua ya maombi kutoka kwa wanafunzi wa kike wa Shule hiyo ya kuomba msaada wa  kuongezewa matundu ya vyoo.

Alisema  kutokana na kutambua upungufu wa shule hiyo  yenye wanafunzi zaidi ya 1000, iliyokuwa na  vyoo Vinne vilivyokuwa vikitumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu.

“Tuliona tutowe msaada ili waweze kupata huduma hii kwa wakati  kwenye ujenzi huu kila  chumba kimegharimu Sh milioni mbili na nusu  kwani vimejengwa kwa ubora  sisi kama taasisi   hufanya zoezi hili kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo  Shule, Miskiti hospitali kwani lengo letu ni  kuhakikisha  tunapunguza changamoto  zinazowakabili”,alisema.

Diwani wa Kata ya Ibungilo, Hussein Magera alisema taasisi hiyo imefadhi zoezi hilo ili kupunguza changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.
Alisema kutokana na upungufu wa matundu ya vyoo taasi hiyo iliona ni vema kutoa msaada huo kwenye shule hiyo ili wanafunzi waweze kupata huduma hiyo kwa wakati.

“Taasisi hii imatujengea matundu 20 yakiwamo ya  wasichana matundu 8 na yawavulana matundu 8 pamoja na walimu matundu 4 ambapo hadi sasa vimekamilika kwa asilimia 90, shule hii inazaidi ya wanafunzi 1000 na mwaka huu tumepokea watoto wa kidato cha kwanza 503 mwaka huu,”alisema Magera.

Hata hivyo alisema wanaendelea na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya walimu ambapo atashakikisha yanalamilika kwa wakati ili wanafunzi waweze kuyatumia pindi shule zitakapofunguliwa.

Alisema Kata hiyo inajumla ya shule mbili za sekondari ikiwamo Ibungilo na Kiloleli ambapo zinakabiliwa na  upungufu wa vyumba 22 vya madarasa.

 “Shule ya kiloleli kuna vyumba vinne vimefikia hatua ya kifunga lenta na ujenzi unaendelea  huku kutoka kwa wanafunzi qa ya Ibungilo  vyumba vitatu vimenyanyuliwa tunatatajia kufunga lenta na kuongeza kozi za juu tumepokea sh milioni 20  ili kukamilisha ujenzi huo.

” Halmashauri  ya Ilemela imeelekeza nguvu kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa lengo la kuhakikisha ifikapo  january 28  changamoto hiyo inakwisha,”alisema Magera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles