26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

WALIOACHA KUTUMIA DAWA ZA ARV’S KUSAKWA

Na Derick Milton – BARIADI


NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile ameiagiza idara ya afya mkoani  Simiyu, kutafuta njia ya kuwapata   zaidi ya watu 10,000 mkoani humo wanaoishi na virusi vya Ukimwi ambao

wanadaiwa kuacha kuhudhuria kliniki.

 

Dk. Ndungulile alisema idadi hiyo ni kubwa  na kuna hatari ya kuongezeko maambukizi mapya ya ugonjwa huo  ikiwa watalaamu wa afya kwa kushirikiana na viongozi watashindwa kuwatafuta na kuwapata   kujua kama wanaendelea na matibabu au wameacha.

 

Naibu Waziri   alitoa agizo hilo jana alipozungumza na  viongozi wa mkoa huo wakiwamo watalaamu wa afya katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo.

 

Alitoa kauli hiyo  baada ya kupata taarifa kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Jumanne Sagini ambaye alisema kati ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi  37,325 walioanzishiwa dawa hizo mwaka 2017   watu  23,339  ( asilimia 62.5) ndiyo wanaendelea kutumia dawa hizo.

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles