28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

CCM YAWEKA KIBINDONI MADIWANI 30

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewapitisha wagombea 30 wa udiwani wa CCM katika uchaguzi mdogo wa kata 77 utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu, ambao wamepita bila kupingwa.

Akizungumza  Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Athumani Kihamia, alisema wagombea hao wamepita bila kupingwa baada ya tume kukutana, kujadili na kuyatolea uamuzi mapingamizi mbalimbali yaliyoweka na wagombea wa udiwani.

Alisema madiwani wote waliopita bila kupingwa wanatoka Chama cha Mapindizi (CCM).

Alisema  rufaa zilipokelewa na kujadiliwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,474FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles