26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu walipwa madeni ya Sh bil 22/-

ndalichakoNA ELIYA MBONEA, ARUSHA

SERIKALI imesema imelipa Sh bilioni 22 za  madeni yasiyo ya mishahara walimu  63,416 wa shule za msingi na sekondari hadi Aprili,mwaka huu.

Hayo yamesemwa  mjini hapa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alipozungumza na maofisa elimu wa shule za sekondari na msingi,wadhibiti ubora wa elimu na wakuu wa shule za sekondari na msingi mkoani hapa.

Alisema Serikali imejipanga kuendelea kulipa madeni yote ya walimu,ukiwa ni utaratibu endelevu, hasa madeni yasiyo ya mishahara.

“Hadi Aprili 14 mwaka huu, walimu 63,416 wa shule za msingi na sekondari wamelipwa madeni yao ambayo ni zaidi ya Sh bilioni 22,” alisema Profesa Ndalichako.

Kuhusu sera ya elimu bure inayotolewa na Serikali, Profesa Ndalichako alisema imelenga kuhakikisha watoto wengi wanapata elimu kwa kadri inavyowezekana.

Alisema kutokana na wazazi na walezi wengi kukosa uwezo wa kifedha wa kuwapeleka watoto wao shule, kulichangia watoto  kukosa haki yao msingi ya kupata elimu.

Alisema mwaka 2015, wanafunzi waliojiandikisha darasa la kwanza waliongezeka kutoka 998,667 hadi 1,341,589  mwaka huu.

“Hii ni ushahidi wa tosha sera ya elimu bure inayotolewa na Serikali imekuwa mkombozi kwa wananchi wa Tanzania, hasa wenye kipato cha chini.

“Serikali inatambua kuwapo dhana yake, wananchi hapaswi kuchangia chochote katika sekta ya elimu jambo ambalo si kweli,’ alisema.

Akirejea waraka namba sita wa elimu wa mwaka 2015, alisema  umeweka bayana majukumu ya wadau wote wa elimu na kuwa wananchi wataendelea kuhusishwa katika kuchangia maendeleo.

Alisema kwa kipindi kirefu, ameendelea kupokea simu za kutaka  ufafanuzi wa sera ya elimu
bure kutoka kwa wananchi mbalimbali.

“Serikali haiko tayari kuona mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa sababu ya michango yeyote, haijawazuia wananchi wenye
mapenzi mema kuchangia sekta ya elimu,”alisema Profesa Ndalichako.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Addoh Mapunda alisema mkoa huo kuanzia Januari mwaka huu, ulipokea Sh biliobi 1.7 kwa ajili ya kugharamia elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles