30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu wafaulu kwa kishindo

Dk Charles Msonde
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk Charles Msonde

Na Mwandishi Wetu

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk Charles Msonde, ametangaza matokeo ya ualimu kwa ngazi ya cheti na stashahada ambapo ufaulu wake ni kati ya asilimia 80 na 90.

Alisema mtihani huo ni ule wa daraja A (Grade A Teacher’s Certificate Examination – GATCE), Stashahada ya Ualimu Sekondari (Diploma in Secondary Education Examination – DSEE) na Stashahada ya Ualimu Ufundi (Diploma in Technical Education Examination – DTEE.

Kwa upande wa Grade A, alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 10,827, kati yake wasichana wakiwa 4,093 sawa na asilimia 37.80 na wavulana wakiwa 6,734, sawa na asilimia 62.20.

Alisema kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, 10,789 walifanya mtihani huo, wasichana wakiwa ni 4,078 sawa na asilimia 99.63 na wavulana walikuwa 6,711 sawa na asilimia 99.66.

“Watahiniwa 38 sawa na asilimia 0.35, wakiwemo wasichana 15 sawa na asilimia 0.37 na wavulana 23 sawa asilimia 0.34 hawakufanya mtihani huo kutokana na kutokulipa ada,” alisema.

Katika kundi hili, alisema jumla ya watahiniwa 10,695, sawa na asilimia 99.62 waliofanya mtihani huo wamefaulu, kati yao wasichana wakiwa 4,049 sawa na asilimia 99.66 na wavulana 6,646, sawa na asilimia 99.60.

Kwa upande wa mtihani wa stashahada ya ualimu, alisema watahiniwa waliosajiliwa kuufanya walikuwa ni 4,931, kati yao wasichana wakiwa 1,698 sawa na asilimia 34.44 na wavulana ni 3,233 sawa na asilimia 65.56.

“Kati ya watahiniwa hao, 4,899 walifanya mtihani huo ambapo 1,685 sawa na asilimia 99.23 ni wasichana na 3,214 sawa na asilimia 99.41 ni wavulana,” alisema Dk. Msonde.

Kati ya watahiniwa hao, 4,161 sawa na asilimia 85.71 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu, kati yao 1,401 sawa na asilimia 83.64 ni wasichana na 2,760 sawa na asilimia 86.79 ni wavulana.

Kwa upande wa stashahada ya ufundi, alisema waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa watatu na wote walishindwa baadhi ya masomo, hivyo watarudia mitihani hiyo mwakani.

MATOKEO YALIYOZUILIWA

Alisema Baraza limezuia matokeo ya watahiniwa 95 ambao walifanya mtihani huo bila ya kulipa ada ya mtihani, ambapo kati ya watahiniwa hao 51 ni wa GATCE na 44 wa DSEE.

Habari hii imeandaliwa na Fredy Azza, Maneno Selanyika, Veronica Romwald na Maria Kaira (RCT), Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles