27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu waeleza walivyokabiliana na moto Shule ya Sekondari Jakaya

Na Renatha Kipaka, Muleba

MWALIMU wa Taaluma katika shule ya Sekon­dari ya Jakaya iliyo­po wilayani Muleba mkoani Kagera, Ayoub Suleman ameeleza jinsi walivyofanikisha ku­zuia moto usiendelee kuteketeza mabweni ya wanafunzi licha ya moto huo kuteketeza mabweni mawili yal­iyokuwa yakitumiwa na wasichana.

Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu Suleman amesema wanafunzi wa­kiwa darasani wakien­dele na kipindi cha dini saa za ji­oni Julai 23, mwaka huu, waliona moto kat­ika mabweni mawili ya wasichana na kuagiza wanafunzi wote ku­toka nje.

“Tuliona moto bweni la kwanza la wasicha ambalo lilikuwa lik­iungua na kuelekea bweni la pili wakati huo wanafun­zi hawakuwa bwenini walikuwa kwenye kipi­ndi cha dini, baada ya kuona hivyo tulifa­nya ushirikiano wa kuokoa vitu kwenye ma­neno mengine,” amesema Suleman.

Amesema hatua ya awali ilikuwa ni kwenye mabweni hayo ilikuwa ni kuitoa ma­godoro, shuka, vitanda daftari za wanafunzi ili kuokoa vifaa hivyo kuteketea na wa­nafunzi kupoteza mali zao.

“Tukitumia vifaa vye­tu vya kujikinga ma moto tukibeba mchang­a, maji wote kwa pam­oja uongozi na baadhi­ ya wanafunzi jasiri tulifanikiwa kushirikiana kudhibiti moto huo ili mab­weni mengine yasiweze kuungua,” amesema Suleman.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema katika tukio hilo bado chanzo cha moto hakijafahamika na hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoto­kea.

Amesema athari iliyoto­kea ni kuungua kwa mali za wanafunzi ikiwamo daf­tari, magodoro, sale za shule vitanda na majengo mawili ambayo yalikuwa yakibeba id­adi ya wanafunzi 62. Mkuu wa Mkoa wa Kag­era, Meja Jenerali Ch­arles Mbuge, amesema ili kubaini tatizo la kuteketea kwa moto huo ameunda kamati itakayo fuatilia un­dani wa ajali hiyo.

Hata hivyo amewataja wanafunzi na walimu kuondoa hofu na sim­amanzi ya kufunguliwa na mabweni​ ya shu­le hiyo kwani vifaa vitapatikana na maso­mo yataendelea kutol­ewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles