30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘Walimu marufuku kuvaa vimini’

mini-skirt-jpgNA OSCAR ASSENGA-TANGA
WALIMU wanawake wa shule za msingi na sekondari mkoani Tanga, wametakiwa kuacha kuvaa nguo fupi  (vimini).

Mratibu wa Mandeleo ya Wanawake Kanda ya Kati (Inuka), David Msuya amesema nguo hizo zinakiuka maadili ya utumishi na kusababisha wanafunzi kushindwa kuzingatia masomo na  kutumia muda mwingi kuwatazama wanapofundisha.

Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema tabia hiyo imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa kushusha ari ya wanafunzi kusoma.

Badala ya kuzingatia wanachofundishwa wanaishia kutazama namna ya uvaaji wa nguo za aina hiyo, alisema.

Alisema   licha ya vimini, pia nguo nyingine ambazo zimekuwa zikiwapa wakati mgumu ni wale wanaovaa madela na baibui ambazo pia zimekuwa zikionyesha maungo kwa urahisi na kusababisha usumbufu kwa jamii.

“Uvaaji wa nguo fupi unasababisha wanafunzi kushindwa kuzingatia wanachokuwa wakifundishwa hasa wakati wanapokuwa wakiinama kwa sababu  baadhi ya maungo yao ya mwili huonekana jambo ambalo linasababisha kuwaondolea umakini wa kusoma,” alisema.

Mratibu huyo alikemea suala la rushwa ya ngono hasa kwenye nafasi ndani ya halmashauri ikiwamo kitendo cha kupendelewa baadhi ya wakuu wa idara
ambao hawastahili.

Alisema   hata usimamizi wa mitihani wa darasa la saba walimu wanaopangwa ni wale wale jambo ambalo huwavunja moyo watumishi wengine ambao hufanya kazi zao kwa weledi mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles