29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Walemavu wanaotokana na ajali waongezeka

Othuman Kiloloma
Othuman Kiloloma

Na VERONICA ROMWALD,  DAR ES SALAAM

KAIMU Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othuman Kiloloma, amesema takwimu zinaonyesha kuwapo ongezeko kubwa la walemavu wanaotokana na ajali nchini.

Dk. Kiloloma alitoa kauli hiyo jana wakati wa hafla ya kupokea msaada wa miguu bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 60.

Alisema msaada huo umetolewa na Taasisi ya Legs 4 Africa ya nchini Uingereza kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hivyo.

“Takwimu zetu zinaonyesha mwaka 2013 tulikuwa tukipokea wagonjwa 15 wa dharura watokanao na ajali, idadi hiyo imeongezeka na sasa tunapokea wagonjwa kati ya 50 – 60 kwa siku,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Kiloloma alisema takwimu hizo zinaonyesha robo tatu ya majeruhi hao ni wale wanaotokana na ajali za pikipiki, maarufu bodaboda.

Alisema wapo wanaokatika mikono na miguu hali iliyofanya kuongezeka kwa uhitaji wa viungo bandia.

“Gharama za utengenezaji wa viungo hivi inategemea vipuri ambavyo hununuliwa nje ya nchi, baada ya utengenezaji mguu mmoja hugharimu kati ya Sh milioni 3.5 hadi sita kutegemeana na uzuri wake, chuma na aina ya ‘joint’ iliyopo pale.

“Hakukuwa na uwiano kati ya vifaa tulivyonavyo na vile vinavyohitajika, gharama yake ni kubwa mno na vifaa tulikuwa tunavichukua toka nchini Ujerumani, kuna gharama ya usafiri kuvitoa kule viliko na hata kuvitoa bandarini vinapofika nchini,” alisema Dk. Kiloloma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles