25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Wabunge wachangia milioni 85/- Kagera

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai.
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai.

Na MAREGESI PAUL, DODOMA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amesema wabunge wamechanga Sh milioni 85.5 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu.

Spika Ndugai alitoa taarifa hiyo bungeni jana baada ya kuhitimisha kipindi cha maswali na majibu.

“Waheshimiwa wabunge, kama mtakumbuka, mwanzoni mwa wiki mlikubaliana kuchangia posho zenu za siku moja kwa ajili ya kuwasaidia wenzetu waliopata madhara yaliyotokana na tetemeko la ardhi kule Kagera.

“Tayari michango yenu imeshakusanywa na zimepatikana shilingi milioni 85, laki tano na elfu themanini.

“Kwa hiyo, tutaziwakilisha panapohusika ili ziweze kuwasaidia wenzetu waliopata matatizo,” alisema Spika Ndugai kwa kifupi.

Septemba 10 mwaka huu, tetemeko la ardhi lilitokea katika mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita na kusababisha madhara makubwa mkoani Kagera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles