30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wakuu wa mikoa wajadili kipindupindu

Dk. Stephen Kebwe
Dk. Stephen Kebwe

Na SARAH MOSES, DODOMA.

WAKUU wa mikoa ya Dodoma na Morogoro, wamekutana ili kujadili namna ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Wakuu hao, Dk. Stephen Kebwe wa Morogoro na Jordan Rugimbana wa Dodoma, walikutana jana wilayani Gairo, mkoani Morogoro baada ya kuitisha kikao cha dharura cha kujadili ugonjwa huo.

Pamoja na viongozi hao wawili, kikao hicho kilihusisha pia viongozi mbalimbali wakiwamo waganga wakuu wa wilaya ambao maeneo yao yamebainika kuwa na ugonjwa huo.

Katika kikao hicho, walikubaliana kuainisha vyanzo mbalimbali vinavyosababisha maradhi hayo vikiwamo maji.

Maazimio mengine ni utekelezaji wa usimamizi wa sheria za usafi wa mazingira ikiwamo ukaguzi wa vyoo na kwamba watakaokutwa hawana vyoo, wapigwe faini na wanaouza vyakula kwenye migahawa katika mazingira machafu, wachukuliwe hatua.

Pia, walikubaliana kuunda mkakati wa pamoja kwa wataalamu wa mikoa hiyo utakaohusiana na maeneo yenye milipuko na kuandaa maeneo ya kuweka kambi kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa maradhi hayo.

Awali, akisoma taarifa ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa Mkoa wa Morogoro, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Frank Jackob, alizitaja wilaya zinazokabiliwa na ugonjwa huo kuwa ni Morogoro, Morogoro Manispaa, Mvomero na Kilosa.

Kwa upande wake, Dk. Kebwe alisema mkoa huo umekuwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kupokea wageni wengi wanaotoka katika mikoa mbalimbali nchini kutokana na magari yanayofika mkoani humo pamoja na uwepo wa mito mingi yenye maji yasiyo salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles