25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mkufunzi CAF awanyooshea kidole waamuzi nchini

Mwamuzi Rajab Mrope, akimlalamikia kipa wa timu ya African Lyon, Youthe Rostand, kwa kupoteza muda wakati wa mechi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi Rajab Mrope, akimlalamikia kipa wa timu ya African Lyon Youthe Rostand, kwa kupoteza muda wakati wa mechi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

MKUFUNZI wa Waamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Leslie Liunda, amemtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Chama, kujitathmini kutokana na matukio ya aibu yanayotokea katika michezo mbalimbali ikiwamo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kauli hiyo ya Liunda inatokana na kitendo cha juzi cha mwamuzi wa mchezo wa Yanga na Mbeya City, Rajab Mrope kutoka mkoani Ruvuma, kutoa uamuzi  wenye utata wa bao la pili la Mbeya City kwenye mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, ambao vijana wa Jangwani walichapwa jumla ya bao 2-1.

Bao hilo lililofungwa dakika ya 36 na Kenny Ally aliyepiga mpira wa adhabu na kujaa wavuni, lilisababisha mpira kusimama kwa dakika tano, baada ya mwamuzi Mrope kutaka kulikataa, lakini baadaye alikubali licha ya kuwa wachezaji wa Yanga kudai Mbeya City walianza shambulizi kabla ya kuruhusiwa na mwamuzi huyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Liunda alisema vitendo vinavyofanywa na waamuzi ni vya aibu katika maendeleo ya mchezo wa soka nchini.

“Alichokifanya Mrope kama angekuwa jijini Dar es Salaam, maisha yake yangekuwa matatani kutokana na uamuzi wa kubabaisha alioufanya katika mchezo huo.

“Lakini mara kadhaa licha ya kulalamikiwa vitendo hivi, hakuna jitihada zozote zinazoonekana kutoka katika Kamati hiyo zitakazokomesha uzembe unaofanywa na waamuzi hao,” alisema Liunda.

Katibu huyo wa zamani wa Kamati ya Wamuuzi nchini, alisema hofu yake ni kuhusu uwezo wa waamuzi kuchezesha mpira na si kuzifahamu sheria 17 za mchezo wa soka.

“Kuchezesha mpira ni jambo jingine ambalo lipo mbali na kufahamu sheria 17 za mchezo wa soka, kwani mwamuzi anaweza kuzijua sheria hizo lakini akawa hafahamu namna ya kuchezesha mpira wenyewe.

“Hata hivyo, kwanini utata wa uamuzi ujitokeze katika michezo ya Yanga zaidi ya timu nyingine na kwanini viongozi wa kamati hiyo wasichukue hatua mapema ili kuinusuru kushuka thamani tasnia hiyo?” alihoji  Liunda.

Mkufunzi huyo pia aliongeza kuwa kama wenye mamlaka wakiendelea kufumbia macho vitendo hivyo, vinaweza kuathiri kiasi kikubwa taaluma hiyo ambayo inaaminika na wapenda soka nchini.

“Vitendo vinavyofanywa na waamuzi wa hapa nchini havifai kuigwa na vizazi vijavyo, kwani vinatishia uhai wa maisha yao na havina sifa ya kuigwa,” alisema Liunda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles