27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kenyatta awaondoa wanajeshi wake Sudan Kusini

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta

NAIROBI, KENYA

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametetea hatua ya nchi yake na kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kikosi cha Umoja wa Mataifa (UN) cha kulinda amani nchini Sudan Kusini.

Rais Kenyatta alisema licha ya Kenya kujitolea kuchangia amani katika kanda hii na dunia nzima, haiwezi kukubali heshima yake ichafuliwe.

Kenyatta alikuwa akizungumza wakati akiongoza hafla ya kufuzu kwa wanajeshi kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Lanet, Kaunti ya Nakuru.

Alisema uamuzi wa kuondoka kwenye mpango huo wa amani unafuatia visa vinavyachafua ujumbe wa UN nchini Sudan Kusini, ambapo umoja huo ulimlaumu kamanda kutoka Kenya.

Kenyatta alisema nchi yake imechangia kutoa makamanda mahiri kuongoza harakati za kulinda amani.

Aliwataja makamanda hao kuwa ni pamoja na Luteni Jenerali Daniel Opande, aliyekuwa Kamanda wa kikosi cha kulinda amani nchini Sierra Leone pamoja na Luteni Jenerali Ngondi aliyeongoza vikosi vya kulinda amani nchini Liberia.

Uamuzi wa Kenya kuondoa jeshi lake unatokana na kuchukizwa na kile ilichoita utaratibu usiofaa wa kumwachisha kazi Jemedari Johnson Mogoa Kimani Ondieki.

Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, alimfuta kazi Luteni Kanali Ondieki, baada ya ripoti ya uchunguzi kusema alikosa kuwajibika kulinda raia wakati mapigano yalipozuka upya nchini Sudan Kusini, Julai mwaka huu.

Ripoti hiyo imesema walinda amani waliokuwa chini ya jemedari huyo hawakuchukua hatua yoyote wakati wanajeshi wa Serikali waliposhambulia kituo cha utoaji misaada mjini Juba na kuwadhulumu raia.

UN hadi sasa haijajibu hatua ya Kenya ya kutokubaliana na uamuzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles