26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wakurugenzi watakiwa kuanzisa mashamba darasa ya pamba

Sheila Katikula, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amewataka Wakurugenzi na Maofisa Ugavi kuhakikisha wanaanzisha mashamba darasa kwa kutumia asilimia 10 ya fedha za mapato ya halmashauri ili kuweza kuimalisha  kilimo cha  pamba.

Mhandisi Gabriel ametoa wito huo Septemba 17, mkoani humo katika kikao cha kampeni ya uhamasishaji wa kuongeza tija katika zao la pamba kilichowakutanisha viongozi mbalimbali na kusisitiza maofisa hao siyo lazima wawe na shamba wanalolimiki wao bali wanaweza kuandaa wakulima wa mfano.

Amesema ili kurejesha thamani ya zao la pamba ni lazima wakulima wajifunze kuzalisha kwa tija na kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu kitu ambacho iwapo kitatiliwa maanani basi huenda uzalishaji wa pamba utaongezeka mara dufu.

Amefafanua kuwa uzingatiwaji wa elimu ya kilimo cha zao la pamba ituwezesha kufikiwa lengo la mkoa kuzalisha tani milioni moja ifikapo mwaka 2025 kwani Mwanza ni miongoni mwa mikoa inayozalisha zao la pamba kwa wingi.

Amesema mwaka 2016/2017 uzalishaji ulikuwa tani 11,531, mwaka 2017/2018 uzalishaji ulikuwa tani 17,376, mwaka 2018/2019 uzalishaji ulikuwa tani 33,010 na 2019/2020 kulikuwa na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo zilipatikana tani 8,039.

Kwa upande wake Balozi wa zao la Pamba nchini, Aggrey Mwanri, amesema jambo kubwa ni kuwawezesha viongozi kuhusu kilimo cha pamba hali itakayowawezeshavkufanya kazi ya kusaidia kuongeza tija kwenye zao hilo.

Amesema ni wajibu kwa viongozi kusimamia na kuhimiza mabadiliko ya kilimo cha zao la pamba kutoka kulima kwa mazoea na kuanza kulima kwa kuzingatia maelekezo ya watalaamu wa kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles