24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WAMLILIA DC SOKO LA KUNDE ALILOWAHAIDI

Na DERICK MILTON

WANANCHI wa Kata ya Nkololo wilayani  Bariadi  wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga, kuwasakia soko la  kunde kama alivyowaahidi kuwasaidia Septemba mwaka jana.

Baadhi ya wakulima hao walisema mkuu huyo wa wilaya aliwaeleza kuwa iwapo watajikita katika kilimo  kunde soko lipo.

Aliwaahidi  kuwasadia watakapovuna, hivyo walikuwa wakimkumbusha kuwa wamefanikiwa kuvuna.

Walikuwa wakizungumza  mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka katika mkutano wa hadhara uliofanyikia viwanja vya CCM.

Walisema kuwa baada ya maelezo ya mkuu wa wilaya walihamasika na kulima  mazao mbalimbali kwa wingi.

Cosmas Kitwima, alisema waliamua kulima dengu, choroko, mbaazi   na alizeti baada ya kuelezwa kuwa soko lipo na bei yake kuwa nzuri lakini baada ya kuvuna na sasa wanahangaika   kupata soko hilo.

“Tumelima, lakini baada ya kulima mazao hayo tunakosa soko la kutosha, bei yake ni kidogo sana.

“Kwa kuwa RC (mkuu wa mkoa) upo hapa na DC, tunamkumbusha lile soko alilotuhaidi liko wapi?”alisema.

Leo Masanja, alisema   wanahitaji soko lenye bei nzuri kwa kuwa wakulima wengi waliolima waliitikia wito wa DC.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Mtaka, aliingilia na kuwaeleza kwamba uamuzi wa DC ulikuwa sahihi hivyo aliwataka kuwa wavumilivu wakati serikali ikiedelea kutafuta soko   na bei kuwa nzuri.

“Mkuu wa wilaya alikuwa sahihi … alitaka msipate njaa, tatizo la bei na soko tunaendelea kulifanyia kazi… sasa niwasihi kutunza hayo mazao yenu soko litapatikana na mtauza kwa bei nzuri zaidi,” alisema Mtaka.

Aliwataka wananchi hao kulima tena mazao hayo kwa wingi wakati serikali ikiendelea kutatua changamoto za bei nzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles