26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi wa Golani-Kimara kuanza mwaka na huduma ya maji

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Mtaa wa Golani uliopo kata Kimara Wilayani Ubungo ndani ya siku kumi na nne.

Waziri Aweso aliyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya Kimara kwa lengo la kutatua changamoto ya upungufu wa maji katika maeneo hayo.

“DAWASA mnafanya kazi nzuri sana, nataka kuona wananchi wa mtaa wa Golani wanapata maji ndani ya siku kumi na nne,” alisema.

“Kwa kuwa mmeweza kufikisha maji kwenye maeneo mengine ndani ya jiji ikiwemo Kifuru kwa gharama kubwa, najua hamtashindwa kufikisha maji kwenye mtaa wa Golani kwa muda huo,” aliongeza Waziri Aweso.

Afisa Atendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja alimhakikishia Waziri Aweso na wakazi wa mtaa wa Golani kuwa wataanza kupata maji ndani ya siku kumi na nne kuanzia leo Desemba 24, 2020.

Mhandisi Luhemeja amesema tayari mabomba ya kusafirisha maji hadi katika eneo la kilomita 3.7 yameshafika eneo la mradi.

“Kutokana na eneo hili la mnazi mmoja kuwa na milima DAWASA imeandaa mradi utakaosafirisha maji hadi katika eneo hilo bila kuruhusu maunganisho mengine njiani. Aliwataka viongozi wa mtaa huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuwa bomba hilo halitakuwa na matoleo ili kuwezesha maji kufika Golani.

“Mpaka sasa tumeshasanifu mradi kwa ajili ya kupitisha mabomba ya maji, kwenye eneo na bomba lina urefu wa kilomita 3.7,” alisema Afisa Mtendaji Mkuu.

Mradi unatarijiwa kunufaisha zaidi ya wakazi wapatao 3,200 wa Golani ambao hawakuwa na maji ya uhakika kutokana na jiografia ya eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles