24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wajawazito mbioni kupata dawa ya kukwepa uchungu

pregnant-woman-outside

VITABU vya dini vinasema, mwanamke atazaa kwa uchungu. Lakini wanawake wa siku hizi tumekuwa hatutaki kuzaa kwa uchungu na badala yake tunafuta dawa na njia mbalimbali kuhakikisha kuwa tunajifungua kwa raha mustarehe.

Wapo wanawake wengine ambao wanadiriki kuwaomba madaktari wawazalishe kwa kisu mara tu mtoto anapotimia ili mradi kukwepa maumivu ya uchungu ambayo mama hukumbana nayo wakati wa kujifungua.

Wakati wanawake wakiamua kuzaa kwa njia ya upasuaji ili kukwepa maumivu ya mtoto kutoka tumboni, wanasayansi nao wamegundua njia mbadala ya kumfanya mwanamke asihisi uchungu wakati wa kujifungua.

Wamegundua kuwa nyoka mwenye sumu kali zaidi duniani huenda akawa jibu la kupatikana kwa dawa ya kupunguza uchungu.

Nyoka anayeitwa ‘Blue Coral’ ndiye mwenye sumu kali zaidi na hupatikana zaidi Kusini Mashariki mwa Bara la Asia. Utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la afya la Toxin umesema nyoka huyo huwalenga maadui wake ambao husababisha uchungu kwa binadamu.

Wanasayansi wanasema huenda sumu hii ikatumika kutengeneza dawa ya uchungu. Baadhi ya wanyama ambao sumu yao imetumika kutengeneza dawa ni pamoja na konokono wa baharini na bui bui wa sumu.

Wanasayansi sasa wanataka nyoka huyu kuhifadhiwa hususan baada ya maeneo mengi anakopatikana kugeuzwa kuwa mashamba ya michikichi. Wanasayansi walifanya utafiti wao katika nchi za China, Singapore na Marekani.

Watafiti wanasema japo kwa mwanadamu nyoka huwa adui, lakini wakati huu huenda akawa suluhu la matatizo mengi ya kiafya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles