30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wajanja wakwapua chakula cha mke wa JPM

janeth-donationNa Judith Nyange, Mwanza

CHAKULA cha msaada kilichotolewa na Mke wa Rais, Janeth Magufuli, katika Kituo cha Makao ya Wazee cha Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza kimeibiwa.

Kutokana na wizi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewaagiza polisi kumkamata msimamizi wa kituo hicho baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kutokana na kupata taarifa kutoka kwa wazee hao kuwa misaada hiyo imekwisha na kwa sasa wanahofia kukumbwa na njaa.

Wizi wa chakula hicho kilichotolewa Machi 6, mwaka huu na Mama Magufuli kwa kushirikiana na Benki ya CRDB, wadau mbalimbali na taasisi binafsi umezua utata juu ya nani mhusika baada ya kutajwa Ofisa Mfawidhi wa kituo hicho, Michael Bundala, polisi na maofisa ustawi wa jamii wa wilaya na mkoa kuhusika na kuibiwa kwake.

Akitoa taarifa ya upotevu wa chakula hicho uliobainika kituoni hapo mbele ya Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mwajuma Nyiruka, alisema baada ya taarifa hiyo walifika kituoni hapo na kubaini upotevu wa tani zaidi ya moja ya unga wa mahindi, tani mbili na nusu za mchele, tani moja ya sukari na vitu vingine vilivyotolewa siku hiyo.

“Uchunguzi wetu wa awali kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama, umebani kati ya tani 12 za unga na mchele zilizotolewa tani 10.8  tu ndizo zimegawiwa kwa wazee hao na tani 1.2  hazijulikani zilipo, katika tani 2.5 ya sukari iliyotolewa iliyogawiwa ni nusu tani tu iliyopo stoo ni kilo 700 na zaidi ya tani 1.2 hazijulikani zilipo,” alisema Nyiruka.

Alisema baada ya msaada huo kutolewa na Mama Magufuli, polisi walilinda msaada huo kituoni hapo kwa muda wa wiki mbili ili kuhakikisha chakula hicho kinahifadhiwa kwa hali ya usalama kisha wakaondoka na ndipo chakula hicho kilipotoweka licha ya kumshauri Bundala kukigawa kwa wazee hao kila wiki.

Alisema baada ya kuzungumza na wazee hao walimweleza kuwa waligawiwa mara mbili yaani Machi 7 na Aprili 7, mwaka huu na walimhoji Bundala kwanini mfuko wa kilo 50 wanagawana watu wawili wakati aliagizwa kuugawa kwa mtu mmoja.

WAZEE WAELEZA

Baadhi ya wazee wanaolelewa katika kituo hicho walizungumza kwa nyakati tofauti kuwa wamewashuhudia askari ambao wamekuwa wakilinda eneo hilo wakitoka na chakula wakati wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi hiyo ya ulinzi na walianza kuwapa shaka kuwa huenda ndiyo ilikuwa sababu ya kugawiwa kidogo.

“Sisi tunashangaa askari polisi ambao wamekuwa wakilinda chakula chetu na wao wakigawiwa na kuondoka nacho, tunajiuliza kwanini wapewe wakati wanalipwa mshahara kwa kazi hiyo,” walisema wazee hao.

Pili wazee hao walisema wamekuwa wakigawiwa chakula hicho kwa kupewa gunia moja la maharage na mahindi  wagawane katika bweni moja wanaloishi wazee 10 pamoja na dumu moja la lita 40 za mafuta na walimuuliza kwanini asiwagawie unga anawapa mahindi bila fedha ya kusaga.

 

MKUU WA KITUO AJITETEA

Kwa upande wake, Bundala, alikiri kuwepo kwa upotevu wa chakula hicho lakini alidai hatambui ni kwa namna gani kimetoweka na akaomba apewe muda ili akifidie.

“Mimi hapa nipo peke yangu lakini sifahamu ni lini chakula kimeibiwa, mambo ya stoo huwa siyafahamu niliomba msaada kwa ajili ya kuingiza takwimu za chakula kilicholetwa, labda kiliibiwa wakati kinaingizwa ghalani, naomba nipewe mwezi mmoja niweze kulipa kwa kuwa kimepotea nikiwa kiongozi,” alisema Bundala.

 

RC ATOA AGIZO

Mongella alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, kumkamata Bundala kwa kosa la wizi kwa kuwa mwenyewe amekubali atalipa na kumtaka Niyiruka kukabidhi taarifa sahihi ya upotevu wa chakula hicho kesho asubuhi ofisini kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles