22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Waislamu wa dhehebu la Shia wapigwa marufuku Nigeria

LAGOS,NIGERIA

SERIKALI ya Nigeria imepiga marufuku Waislam wa dhehebu la Shia wanaoungwa mkono na Iran, kwa madai ya kusababisha vurugu nchini humo na kulitaja dhehebu hilo kuwa ”adui wa taifa”

Vuguvugu la Waislamu nchini Nigeria (IMN) limepinga hatua hiyo serikali likisema linaendesha shughuli zake kwa amani na kwamba serikali imekuwa ikipanga njama dhidi yake.

Hatua hiyo imesababisha hali ya taharuki na hofu ya kuzuka kwa mzozo kati ya Waislamu wa Kishia na Wasunni katika taifa hilo la Afrika lenye utajiri wa mafuta.

Kundi la IMN lilibuniwa miongo minne iliyopita na limekuwa likishinikiza kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa kidini wa Iran nchini Nigeria.

Linachangia pakubwa mapinduzi ya Iran yaliyomsaidia Ayatollah Khomeini kuchukuwa uongozi wa taifa hilo mwaka 1979 baada ya kupinduliwa kwa utawala wa Shah uliyokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Khomeini bado ana ushawishi mkubwa kwa kundi hilo.

Wafuasi wa IMN walitangaza uaminifu wao kwake katika mkutano na baadae kwa kiongozi wao, Sheikh Ibraheem Zakzaky ambaye yupo gerezani kwa mauaji.

Kundi la IMN ambalo linajichukulia kama serikali,  kitendo cha kuzuliwa kwa Sheikh Zakzaky tangu mwaka 2015 kimeamsha maandamano  na hatua hiyo imekuwa kama chanzo cha wao kutaka mamlaka nchini Nigeria.

Wakati serikali ya Nigeria ikichukua uamuzi huo, jana Mahakama ilimruhusu Sheikh Zakzaky kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu.

Wafuasi wake wanasema Sheikh Zakzaky alishambuliwa na kiharusi mara mbili na amepoteza kuona.

Mahakama imewataka watu watakaomsindikiza kwenye matibabu nchini India kuhakikisha anarejea baada ya kupatiwa matibabu.

Kundi hilo la IMN halitambui mamlaka ya serikali ya Nigeria na linachukulia viongozi wa taifa hilo Waislamu na Wakristo kuwa mafisadi na wasiomcha Mungu.

Kumekuwa na makabiliano makali kati ya wafuasi wa IMN na vikosi vya usalama vya Nigeria katika wiki za hivi karibuni.

Kundi hilo lina matawi na mfumo wa utawala katika majimbo 36 ya Nigeria hali inayoipatia sifa ya serikali.

IMN pia linaendesha shule zake na hospitali katika baadhi ya majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria yaliyo na waislamu wengi.

Vugu vugu hilo la Kiislam limesajili Wakfu unaofahamika kama Fudiyya ambao unaendesha jumla ya shule 360 za msingi na sekondari.

“Wakfu hii inaipunguza mzigo serikali lakini inaashiria kuwa serikali haina uwezo wa kutoa elimu kwa watu wake,” ilisema katika tuvuti yake.

Baadhi ya wanachama wake wanasadikiwa kuwa wataalamu na wasomi, huku wengine wao wakishikilia nyadhifa katika jeshi, polisi na idara ya intelijensia.

Jacob Zenn, mchambuzi wa Marekani kutoka wakfu wa Jamestown, anasema kushirikishwa kwa wanachama wa IMN katika huduma ya umma inaonyesha kwamba inasaidia “mageuzi ya Kiislam”, badala ya mapinduzi, nchini Nigeria.

IMN ni kundi kubwa zaidi la Kishia nchini Nigeria.

Lina uwezo wa kuvutia umati mkubwa wa watu katika mikutano yake-wakati mwingine maelfu ya watu hukusanyika katika shughuli zake.

Hii ni kutokana na hatua ya Sheikh Zakzaky, ambaye alichangia kukua kwa dhehebu Kishia katika taifa lililokuwa na na idadi ndogo ya Washia kabla ya mapinduzi ya Iran.

Kundi la IMN limekuwa likifanya maandamano tangu kiongozi wake alipokamatwa na kuzuiliwa mwaka 2015

Washia wanakadiriwa kuwa kati ya asilimia 5 hadi 17 ya Waislamu ambao wanakadiriwa kuwa karibu milioni 100.

Waislamu wengi nchini Nigeria ni Wasunni, sawa na wale wa Saudi Arabia au Misri.

Ofisi ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari imesema kundi la IMN limepigwa marufuku kwa sababu limetekwa na watu wasioamini maandamano ya amani na badala yake linatumia ghasia kufikia malengo yake.

IMN yenyewe linalaumu vikosi vya Nigeria kwa kutumia nguvu kuvunja maandamano ya amani

Hii ni kutokana na mandamano ya wiki kadhaa yaliopangwa na kundi hilo kushinikiza kuachiliwa huru kwa kwa kiongozi wake Sheikh Zakzaky, ambaye amekuwa kizuizini tangu mwaka 2015, na kupigania haki ya mamia ya wafuasi wake waliouawa na vikosi vya serikali.

Baadhi ya maandamano hayo yamekubwa na makabiliano makali kati ya waandamanaji na na vikosi vya usalama,nje ya majengo ya Bunge la kitaifa.

Ofisa wa polisi wa ngazi ya juu ni mmoja wa waliouawa katika mji mkuu wa, Abuja.

Vugu vugu la IMN limekanusha madai ya kuhusika na ghasia na kulaumu vikosi vya usalama kwa mauaji ya watu waliokuwa wakishiriki maandamano ya amani .

Kundi hilo linamchukulia Rais Buhari – ambaye ni Muislamu wa dhehebu la Sunni – kama kibaraka wa Saudi Arabia, na linamshtumu kwa kutaka kuangamiza Washia nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles