33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Democrat wamtupia lawama Trump kuchochea mauaji

WASHINGTON, MAREKANI

WAGOMBEA urais wa chama cha Democrat nchini Marekani wamemlaumu Rais Donald Trump baada ya kutokea visa viwili vya mashambulizi ya bunduki vilivyosababisha vifo vya watu 29 Texas na Ohio.

Wagombea hao wanasema matamshi ya Trump ya kibaguzi dhidi ya walio wachache nchini humo yanachochea mgawanyiko na machafuko.

Katika mikutano ya umma na hata kwenye televisheni wagombea kadhaa wamezungumzia haja ya kuwepo kwa sheria kali za udhibiti wa bunduki.

Pamoja na hayo wanasiasa hao wameelekeza kiasi kikubwa cha lawama zao kwa Trump wakisema mashambulizi hayo ya Dayton na El Paso yana uhusiano na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwa miezi sasa dhidi ya wahamiaji na watu watu wasio wazungu.

Seneta Bernie Sanders amesema “Namwambia Rais Trump, tafadhali achana na matamshi ya kibaguzi dhidi ya wahamiaji, wachana na chuki inayoshuhudia nchi hii ikitumbukia katika machafuko tunayoyaona.”

Rais Trump mwenyewe amelaani mashambulizi yote mawili.

“Ninachotaka kusema ni kwamba hizi ni sehemu mbili nzuri na tunawapenda watu wake. Chuki haina nafasi katika nchi yetu na tutalishughulikia suala hilo,” alisema Trump.

Alipoulizwa kuhusiana na hatua atakazochukua baada ya tukio hilo la mauaji, Trump alisema;

“Tumefanya mengi zaidi kuliko tawala zilizopita na jambo hilo halizungumziwi sana, lakini tumefanya mengi kusema kweli. Lakini labda mengi zaidi yanastahili kufanyika.”

Watu 20 waliuwawa katika duka la jumla la Walmat mjini El Paso huko Texas na polisi wanasema kisa hicho kitachukuliwa kama ugaidi wa ndani ya nchi wakati ambapo wanachunguza madai ya shambulizi lililotokana na chuki.

Mshukiwa wa tukio hilo, Connor Betts e huenda akahukumiwa kifo iwapo atapatikana na hatia.

Polisi pia inasema haijui bunduki hiyo iliponunuliwa ingawa inasema pia kuwa sheria za Texas zinakubali kubeba bunduki kubwa katika sehemu ya umma.

Wakati hayo yakijiri wanafunzi waliokuwa darasa moja na Connor Betts huko Ohio wanasema kuna wakati alifukuzwa shule baada ya kuandika orodha ya watu anaotaka kuwauwa na orodha nyingine ya wasichana anaonuia kuwabaka.

Kauli hizo za wanafunzi hao zimekuja baada ya polisi kusema kuwa hakukuwa na taarifa yoyote mbaya ambayo ingeweza kumzuia mshukiwa Connor Betts kununua silaha hiyo aliyoitumia kufyatua risasi nje ya baa iliyokuwa imejaa watu.

Aliyefanya shambulizi la Dayton Ohio aliuwawa na polisi.

Mexico kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje imesema inapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu aliyemuuzia mshambuliaji huyo silaha kwani raia sita wa Mexico ni miongoni mwa waliouwawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles