23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wahasibu kukutana JNICC

Faraja Masinde- Dar es salaam

CHAMA cha Wahasibu Tanzania (TAA) kinatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa kawaida wa 37 Novemba 12-13, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho, CPA. Peter Mwambuja alisema mkuatano huo kwa mwaka huu utakuwa na kaulimbiu ya “Ushiriki wa Wahasibu kwenye Uendelevu wa UchumiwaKipato cha Kati Tanzania: Fursa, ChangamotonaNamnayakusongambele”.

Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na kwamba baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na Ripoti ya mwaka ya Baraza la UongoziTaifa; Hesabu zilizokaguliwa za Mwaka wa Fedha uliopita; Mabadiliko ya Katiba ya Chama cha Wahasibu; na menginevo.

“Mbali ya Mkutano wa MwakawaKikatiba, kusudi lingine la kusanyiko hili ni kujenga maarifa kwa wahasibu na wakaguzi juu ya umuhimu wao kushiriki katika uendelezaji wa Uchumi wa Kati wa Tanzania.

“Pia kutakuwa na mada muhimu zitakazowasilishwa na wanataaluma ya uhasibu wenye uzoefu mkubwa kwenye taaluma hii waliolitumikia na wanaoendelea kulitumikia taifa hili.

“Miongoni mwa watoa mada ni, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, CPA Ludovick Utouh, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi, CPA Pius Maneno, na neno kutoka kwa CPA Meja Jenerali Mathew Mkigule kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na wengine wengi,” alisema CPA Peter Mwambuja.

Alisema tukio hilo litakuwa ni jukwaa la wadau mbalimbali wa taaluma hiyo kuonyesha huduma mbalimbali ikiwamo uzoefu huku gharama ya ushiriki ikiwa ni Sh 200,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles