Na Tunu Nassor – Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba amewataka wataalamu kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) kutafuta mbinu ya kuvuna maji ya mvua ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vyanzo vya maji.
Kate ameyasema hiyo leo Juni 4, mwaka huu katika ziara ya kamati ya siasa ya Ccm mkoa wa Dar es Salaam walipotembelea miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka hiyo.”Tuna wahandisi wengi Dawasa tujiandae kuja na mawazo ya jinsi ya kuokoa maji ya mvua yanayopotea Bahraini na kutuacha na shida ya maji,” amesema Kate.
Amewapongeza Dawasa kwa kubana matumizi kutoka vyanzo vya fedha vya ndani na kuwekeza katika miradi ya maji.
“Niwashukuru kwa kujibana asilimia 35 ya mapato yenu na kutekeleza miradi huku kutumia ‘false account’ kwa kujisimamia wenyewe na kutekeleza miradi kwa kiwango bora,” amesema Kate.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo amesema mahitaji ya maji yanazidi kuongezeka na yanatarajiwa kufikia lita za ujazo Bilioni moja kwa siku.
“Tufikirie kujenga tenki kubwa kila manispaa kwa ajili ya kuhifadhia maji lenye ukubwa wa kuhifadhi lita za ujazo 100,000 ili kusaidia changamoto za kiangazi kukosemana maji,”amesema Profesa Mkumbo.