24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

WAHAMIAJI ZAIDI YA 50 WAKAMATWA MWEZI HUU MKOANI TANGA

NA OSCAR ASENGA, TANGA

Zaidi ya wahamiaji haramu 50 raia wa Ethiopia wamekamatwa
eneo la Duga wilayani Mkinga mkoani Tanga mwezi huu kutokana na operesheni zinazoendeshwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini.

Hayo ni kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga, DCI Crispian Ngonyani, aliyezungumza na Mtanzania Digital ofisini kwake ambapo alisema wahamiaji hao hivi sasa wanaendelea na kesi zao kutokana na kuingia nchini kinyume na utaratibu uliopo.

Alisisitiza kuwa hatua ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao inatokana na kuwepo kwa misako ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali hasa ya mipakani mkoani Tanga ambapo wahamiaji hao wamekuwa wakitumia kama njia ya kuingilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles