24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

BENKI YA NMB YAZIDI KUNG’ARA KWA UBORA AFRIKA

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam


BENKI ya NMB PLC imeshinda tuzo mbili katika sherehe za utoaji wa tuzo wa benki bora duniani zilizofanyika  London,  Uingereza.

NMB imetajwa kwa mara ya kwanza kuwa ni benki bora ya maendeleo barani Afrika huku tuzo ya pili iliwa ni Benki Bora Tanzania  kwa mwaka  2017. Niyo ni  mara ya tano mfululizo.

Tuzo za umahili za Euromoney 2017hutolewa kila mwaka na huandaliwa na Jarida la Euromoney  na kuyatambua zaidi ya makundi 20 ya bidhaa za  taasisi za  fedha zikiwamo benki kote duniani kwa kuangalia benki bora na ya kiwango cha juu kwa kila bara na benki bora katika nchi takriban 100 duniani kote.

Hivi karibu benki hiyo ilitangazwa benki bora Afrika na kutunukiwa tuzo hiyo ambayo huzitambua taasisi za fedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika maeneo yao kwa kuonyesha ugunduzi na kupata mafanikio ya fedha kila mwaka.

Jarida ya Euromoney liliandika kuwa “NMB siyo benki iliyo hai bali ni benki inayofanya kazi. Uamuzi mkubwa uumekuwa ukifanyika kwenye maeneo ya mtaji, biashara na watu. Katika maboresho hayo, bado benki imeweza kutoa gawio zuri kwa wanahisa kuliko taasisi yoyote ya fedha nchini”.

Akizungumzia ushindi wa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB,  Ineke Bussemaker alisema  ubunifu katika huduma, teknolojia na uwekezaji katika fedha za elektroniki kwa msaada wa mtandao mpana wa matawi na ATM vimechangia kuiboresha benki na kuifanya taasisi bora ya fedha nchini.

“Kutatua changamoto za jamii ya watu wasiotumia huduma za benki nchini inachukua uwekezaji, ubunifu na uwezo wa kuwaleta wadau katika malipo na huduma nyingine za fedha.

“Kuwa ushindi wa tuzo mbili kwa mpigo za benki ya maendeleo Afrika na Benki Bora Tanzania ni kielelezo tosha kuwa juhudi zetu zinaonekana situ Tanzania bali Afrika nzima.

“Tunatoa shukrani zetu wa wateja, wafanyakazi na wadau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa kwa benki,” alisema Ineke na kuongeza kuwa NMB itaendelea na ahadi yake ya kuwapa huduma bora wateja wake sasa na siku zijazo.

Akizungumza kwenye hafla, Mhariri wa Jarida la Euromoney,   Clive Horwood alisema, “Mchuano wa kupata tuzo mwaka huu ulikuwa wa ushindani sana katika taasisi zilizoshiriki na hivyo kufanya uamuzi kuwa mgumu.  Benki zilizoshinda na kujipatia tuzo zetu zimechukua hatua kubwa katika mipango yao ya benki.

“Benki   miaka ya ijayo zitakuwa zinaangalia nini unafanya na pia nini ambacho hukifanyi. Mwaka huu, benki zilizong’ara zimetafsiri kwa kinagaubaga ni wapi kwenye nguvu zaidi na kuzingatia maeneo hayo,” alisema.

Kutokana na umuhimu wake NMB imeendelea kuja na ubunifu wa kila aina katika huduma zake ikiwemo kuja na huduma kwa watoto kwa kuwafungulia akaunti ili waweze kutunza fedha zao zitakazowasaidia hapo baadaye.

Akizungumzia umuhimu wa mpango huo, Mratibu wa Elimu ya Fedha wa NMB,  Ryoba Mkono, anasema mpango wa kufungulia akaunti watoto ulianza Agosti, mwaka jana na kwa sasa mwitikio wake umekuwa mkubwa.

Anasema kuna akaunti za aina mbili, ikiwa ni pamoja na NMB mtoto akaunti, ambayo haina ATM kadi na inakuwa chini ya uangalizi wa wazazi kwa asilimia 100, lakini kuna NMB Chipukizi akaunti, hii ni kuanzia

miaka 13 -18, mtoto anapewa kadi na kujitunzia fedha zake yeye mwenyewe.

Huduma ya NMB Chipukizi akaunti mtoto anatunza fedha zake na anaruhusiwa kutoa kuanzia kiwango cha Sh 5,000 hadi 50,000 na akitoa mzazi wake anatumiwa ujumbe wa meseji kwamba zimetolewa fedha.

“Huduma hii ya watoto ni nzuri sana na huwasaidia watoto kujifunza jinsi ya kuweka akiba kwa matumizi ya baadaye, lakini NMB tunazunguka mashuleni kuweza kutoa elimu hiyo kwa walimu na wanafunzi wao pia,’’ anasema Mkono.

Kutokana na huduma hiyo, mzazi anaweza kumuwekea mtoto wake fedha bila kwenda kwenye tawi lolote akatumia simu na kuweka fedha katika akauti husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles