24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI 31 WAPATA UJAUZITO

Na TIMOTHY ITEMBE -TARIMEMADIWANI wa Halmashauri ya Rorya mkoani Mara, wamesikitishwa na kitendo cha watoto wa shule kupata ujauzito.
Akizungumza mbele ya madiwani wenzake, Diwani Viti Maalumu Tarafa ya Nyancha, Pendo Odele (Chadema), alisema kwa kipindi cha robo ya kwanza katika mwaka 2016/2017, jumla ya watoto 31 katika shule za msingi na sekondari wamepata ujauzito wilayani Tarime.

Odele ambaye alionekana kukerwa na matukio hayo kuendelea kutokea kwa jamii, huku wazazi na watuhumiwa wakielewana kienyeji bila kufikishwa katika vyombo vya sheria, alisema umefika wakati wa hatua kali kuchukuliwa.
“Kitendo cha watoto kuendelea kupata mimba, inaonekana ni jinsi gani wazazi, viongozi na jamii isivyojali na kutambua umuhimu wa elimu kwa mtoto, tunashuhudia mtoto wa kike anapata ujauzito, lakini pande mbili za kijana na binti zinakutana na kumalizana kienyeji, isitoshe majirani wanajua, lakini wanakaa kimya,” alisema.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Bukwe, Charles Wembe (CCM), alisema umefika wakati wa viongozi kuwa kitu kimoja kupambana na wimbi hilo la mimba shuleni na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuhusika na kukatisha ndoto za watoto.
“Mimi binafsi ndani ya kata yangu nimesema kuwa mtu ambaye atabaini kuwa binti amepata mimba na kumtambua kijana aliyehusika, atazawadiwa Sh 50,000 papo hapo baada ya kutoa taarifa ambayo itakuwa sahihi,” alisema.
Wembe aliongeza kuwa kutoa fedha hizo kwa atakayebaini vitendo vya ukatili huo, kutachingia kukomesha au kuwaumbua wote ambao hufanya vitendo hivyo kuwa vya siri.

Naye Mary Thomas (Chadema), Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Kitembe, alisema kuwa watoto wa shule wanapata mimba kutokana na vishawishi vingi njiani, hususani kutoka kwa waendesha pikipiki wanaowadanganya kuwapa usafiri wa bure.
“Kwa pamoja tunahitaji kuungana kupiga vita mimba mashuleni kwa sababu watoto wanaoharibiwa masomo ni wetu na wanaharibiwa maisha na kuzima ndoto zao za baadaye,” alisema Thomas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles