Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba za Asili Tanzania (Shivyatiata), Abdulrahman Lutenga, amewataka waganga wote nchini kuwafichua wenzao waonajihusisha na vitendo vya upigaji ramli chonganishi na kuwatakasa majambazi.
Lutenga alikuwa akizungumza na waganga wa tiba asilia wilayani Maswa jana.
Alisema ili kutatua changamoto zilizopo ni vema kukawa na utaratibu wa kuchunguzana na kutambuana katika kazi zao.
Bila kuwafichua waganga wanaosaidia uhalifu, wote wanaweza kuhesabiwa kuwa wahalifu, alisema.