27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wafugaji waipongeza serikali kutenga malisho ya mifugo

Mwandishi wetu, Arusha

Wadau wa sekta ya mifugo nchini, wamepongeza m
pango wa serikali wa kutenga hekta milioni sita kwa ajili ya malisho ya mifugo nchini, lakini wametaka maeneo hayo yaheshimiwe.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi kiwanda cha maziwa cha Kahama fresh wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera, alisema serikali imejipanga kutenga hekta milioni sita za malisho ifikapo 2025 na tayari hekta milioni 1.5 zimetengwa.

Wakizungumza na matukio, baadhi ya wafugaji na asasi za kutetea jamii za wafugaji wa asili na maliasili,wameeleza,wanaunga mkono mpango wa serikali kuanza kutenga maeneo ya malisho ambao utasaidia sana kupunguza migogoro ya wafugaji na wakulima na taasisi nyingine ikiwepo za uhifadhi.

Mkurugenzi wa mtandao wa mashirika ya wafugaji , wawindaji wa asili na waokota matunda (PINGOs Forum),Edward Porokwa alisema wanaunga mkono mpango mzuri wa kutengwa maeneo ya malisho ya mifugo nchini lakini ni muhimu yaheshimiwe.

Porokwa alisema kuna tatizo kubwa katika kuheshimu maeneo yanayotengwa kama malisho ya mifugo kwani hadi sasa kuna vijiji vimekuwa vikitenga maeneo hayo lakini yamekuwa yakivamiwa na kusababisha migogoro.

“Tunapongeza serikali kwa uamuzi huu lakini tunaomba maeneo yaliyotengwa yaheshimiwe na vyombo vingine kwani yamekuwa yakipungua kutokana na kuanzishwa hifadhi na kuvamiwa na wakulima na shughuli nyingine,”alisema

Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF), Zakaria Faustine, alisema mpango wa kutengwa Maeneo ya malisho upo kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 na hadi sasa karibu hekta 1.5 milioni zimetengwa, utasaidia sana sekta ya mifugo nchini.

Alisema tatizo kubwa la wafugaji nchini ni usalama na uhakika wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao na mambo mengine hata wasipopata wanauwezo wa kutafuta kwa nguvu zao ikiwepo kujenga shule na zahanati.

Mfugaji, Raphael Laizer alisema kama serikali itafanikisha mpango wa kutenga maeneo ya malisho migogoro baina yao na wafugaji na hifadhi itakuwa imepungua sana.

“Watuwekee maeneo ya malisho sisi tupo tayari hata kulipia tulishe mifugo yetu kwani ndio tatizo kubwa kwetu kwani maeneo yetu mengi ya asili yamechukuliwa kufanywa hifadhi mengine kuwa mashamba,” alisema.

Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi, ambapo ina jumla ya Ng’ombe 33.4 milioni, mbuzi 21.3 milioni, kondoo 5.6milion na punda 657,387.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles