30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘WAFANYAKAZI TANZANITE ONE HUKAGULIWA SEHEMU ZA SIRI’

SERIKALI imekiri kuwapo udhalilishaji wanaofanyiwa wafanyakazi wa Tanzanite One mkoani Arusha, kwa kukaguliwa sehemu zao za siri.

Kauli hiyo, ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, Anthony Mavunde wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Joyce Mukya (Chadema).

“Kumekuwa kunafanyika udhalilishaji mkubwa kwa wafanyakazi wa Tanzanite One, wanakaguliwa sehemu za siri hasa sehemu ya kujisaidia haja kubwa, je Serikali inatuambia nini na inachukua hatua gani juu ya udhalilishaji huu,”alihoji Mukya.

Akijibu swali hilo, Mavunde alikiri kuwapo changamoto ya udhalilishaji, huku akisema ameelezwa na wafanyakazi wa mgodi huo baada ya kuwatembelea.

“Mheshimiwa Naibu Spika, anachokisema mbunge ni kweli na nilienda kutembelea huo mgodi,nikakutana na changamoto hiyo kubwa na wafanyakazi walinieleza.

“Tulitoa maelekezo kwa sababu ziko taratibu za kisheria za kufuatwa wakati wa ukaguzi,kama vitendo hivi vinaendelea basi tutachukua hatua za kisheria zaidi,”alisema Mavunde.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Ritha Kabati (CCM) naye aliuliza swali la nyongeza akihoji:”adhabu gani ambayo wanapatiwa hawa wawekezaji kwa sababu jambo hili limekuwa likijirudiarudia.

Akijibu hilo, Waziri Mavunde alisema kila mwekezaji anayekuja kuwekeza nchini anapaswa kufuata sheria.

“Sisi kama Serikali tumekuwa tukichukua hatua. Tumetafsiri sheria kichina, baada ya kuwapo mkanganyiko kwa wawekezaji wa kichina, lakini bado kuna watu wanakiuka taratibu hizi.

“Tunatoa wito kwa wawekezaji wanaokiuka, tutaendelea kuchukua hatua stahiki na adhabu ambayo tumekuwa tukiwapa, tumekuwa tukiwaondoa nchini pale tunapowabaini kuwadhalilisha wafanyakazi,”alisema Mavunde.

Awali akiuliza swali la msingi, Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu (CCM), alitaka kujua lini Serikali itafanya ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini.

Pia alihoji ni kwanini Serikali isiamue kuwaondoa nchini waajiri wakorofi kwa unyanyasaji wanaoufanya.

Akijibu hilo, Waziri Mavunde alisema waajiri wote,yakiwamo na makampuni ya madini wanapaswa kutekeleza matakwa ya sheria za kazi kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi.

Kuhusu ukaguzi wa mikataba zinazofanya kazi migodini, alisema Serikali iliunda kikosi kazi ambacho kilishirikisha maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, NSSF, SSRA, OSHA na Mamlak ya Mapato Tanzania pamoja na Wakala wa Ukaguzi wa Madini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles