26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

MAREKANI YAMPUUZA MWENYEKITI TUME YA AFRIKA

WASHINGTON, MAREKANI


MWENYEKITI wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki, 'alipuuzwa' na Marekani wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mjini Washington.

Kwa mujibu wa Jarida la Sera ya Kigeni (FP), Faki alikuwa amealikwa nchini hapa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson wiki iliyopita, lakini Ofisi ya Tillerson haikuthibitisha mkutano huo na ikawasiliana naye wakati akiondoka kuelekea mjini New York.

FP limeripoti kuwa Wizara ya Mambo ya Nje badala yake ilitaka Faki kufanya mkutano na ofisa wa ngazi za chini hatua iliyomkasirisha na hivyo kufutilia mbali ziara yake yote ya Washington.

Akihojiwa na FP, Balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Afrika (AU), Reuben Brigety, aliukosoa utawala wa Rais Donald Trump kuwa unafanya makosa makubwa au pengine hauoni uhusiano kati yao na Afrika kuwa kitu muhimu.

“Huu ni ujinga katika kipindi hiki ambacho bara la Afrika linaendelea kutafakari kuhusu chaguo lao katika ushirikiano wao duniani,” alisema.

Brigety aliongeza kuwa si mara ya kwanza kwa utawala huo kupuuza viongozi wa Afrika.

Ripoti zinasema kuwa Machi mwaka huu, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, alizuru Washington na hakuna mtu kutoka wizarani au Ikulu aliyekutana naye.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles