31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

MASAUNI: CUF WALIOCHOMA NYUMBA YA KAMISHNA

BUNGE limeelezwa kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa waliorusha bomu katika nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar,  ni viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF).

Kauli hiyo, ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Gando, Othman Omar Haji (CUF).

“Kwanini wafuasi wa CCM waliochoma moto nyumba za Tumbatu hawajakamatwa na pia mikutano ya CCM, imekuwa ikilindwa na polisi wakati ya upinzani huambiwa kuna taarifa za kiintelijensia,”alihoji Haji.

Akijibu swali hilo, Masauni alisema waliochoma nyumba hizo ni wafuasi wa CUF kwa kuwa hata nyumba ya kamishna iliyorushiwa bomu walifanya wao.

“Baada ya uchaguzi kumalizika, viongozi waandamizi wa CUF walikuwa wanachochea wanachama wao kufanya mambo yanayokiuka sheria, ikiwamo kuchoma nyumba ya kamishna na katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi imebainika ni viongozi waandamizi ndio waliofanya hivyo,”alisema Masauni.

Hata hivyo,jeshi hilo limekamisha uchunguzi  wake na kesi itapelekwa mahakamani hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wafuasi wa CCM katika Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, wanatuhumiwa kumteka Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi, Juma Mtanda na kumpora kitendea kazi chake aina ya Ipad.

Tuhuma hizo zilitolewa bungeni jana na Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema), wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo alisema askari polisi wanawafahamu watekaji hao na wamewafumbia macho.

Alisema walitenda makosa hayo wakati wa uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa mitaa na vitongoji na kwamba baada ya mwandishi kupeleka taarifa polisi, askari walifuatilia na kumrudishia mwandishi huyo Ipad yake.

“Mheshimiwa Naibu Spika, hii inamaanisha askari wanawafahamu wahalifu hao, mpaka sasa hakuna kesi wala hatua yoyote iliyochukuliwa,”alisema Lijualikali.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles