25.5 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabishara Geita waipongeza BRELA

Na Anna Ruhasha, Geita

Wafanyabiashara mkoani Geita wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kuboresha hatua za usajili wa alama za biashara na huduma pamoja na hatua za usajili kwa njia ya mtandao kuwa njia hiyo itapunguza changamoto ya kuchelewa kupata huduma kwa wakati.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano BRELA, Roida Andusamile akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwepo katika manaonesho ya tano ya teknologia ya madini mkoani Geita.

Wakizungumza na Mtanzania Digitil kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda waliotembelea Banda la BRELA katika maonyesho ya tano ya Teknolojia ya Mdini yanayoendelea mjini Geita.

Mmoja wa wafanyabiashara hao ni Meriness Johan nambaye amesema usajili wa njia ya mtandao umewasaidia kupata huduma kwa haraka tofauti na miaka ya nyuma.

“Kiukweli sasaivi serikali imekuja na mwarobaini maana tulikuwa tunazunguka sana kuja kupata usajili mpaka tulikuwa tunakata tamaa kwa sasa ni wewe na mtandao, tunaishuru serikali ya mama Samia pia BRELA kwa kuturahisishia huduma,” amesema Johan.

Afsa Tehama kutoka BRELA, Andrew Godfrey amewakumbasha watanzania kuwa huduma za wakala za usajili zinatolewa kwa njia ya mtandoa huku akiwataka wananchi kutumia maonesho ya tano ya teknologia ya madini kufika banda la BRELA kusajiliwa pia na kupewa cheti cha usajili.

“Tangu maonesho ya tano ya teknolojia ya madini yameanza hapa mkoani Geita BRELA kupitia mfumo ORS tumesajili wateja 25 kwa njia ya mtandao lakini pia tunasajili alama za Biashara, Kampuni ‘Leseni za viwanda na huduma nyingine ikiwamo ushauri,” amesema Godfrey.

Amewasihi wakazi wa Geita na maeneo ya jirani kutumia fursa ya maonyesho hayo kukamilisha urasmishaji wa biadhara zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles