30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapongeza mchango wa Taasisi za Dini katika kuleta maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

“Serikali inatambuamchango wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya katika maendeleo ya Sekta ya Elimu kupitia taasisi zake za elimu; Sekta ya Afya kupitia hospitali na namna mnavyojitolea kuchangia damu salama katika benki ya taifa ya damu; pamoja na sekta ya maji kupitia mpango wenu wa kuchimba visima vya maji maeneo mbalimbali nchini,”.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 51 wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam Septemba 30, 2022 Wzairi wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene wakati wa uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 51 wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya Tanzania kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa aliyekuwa Mgeni Rasmi.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu anawapongeza, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry – Amir na Mubashir Mkuu, pamoja  na Wasaidizi wako wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya kwa uongozi mahiri unaolenga kudumisha Amani na Utulivu hapa nchini, kupitia kaulimbiu yenu ya, Upendo kwa wote bila chuki kwa yeyote,” amesema Simbchawene.

ameongeza kuwa: “Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ustawi wa Taasisi hizo ili ziendelee kuwa sehemu ya kuliletea maendeleo Taifa letu,” amesema Simbachawene na kuongeza kuwa:

“Nyote mnatambua kuwa nchi yetu kupitia ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977 haiegemei upande wowote katika masuala ya dini – Secular State. Hata hivyo, sehemu kubwa ya watu wake wanaamini katika Mungu kupitia dini zenye madhehebu mbalimbali.

“Kwa msingi huu, nchi yetu kupitia ibara ya 19 ya Katiba, inatambua uhuru wa kuabudu kwa mtu mmoja mmoja au kundi la watu katika madhehebu na dini zao ili mradi tu wafuate masharti ya Katiba na Sheria za Nchi,” amesema Simbachawene.  

Waziri George Simbachawene akitembelea moja ya  banda la vitabu la Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya.

Aidha, amewasishi katika siku zote tatu kuendelea kuliombea taifa la Tanzania amani, utulivu, upendo na mshikamano.

Naye Naibu Ami, Shekhe Abdurahman Mohamed amesema Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya inashika mafundisho ya Kiislamu kwa usahihi wake.

“Shida inakuwepo pale waumini wanapofundishwa dini na wakaiacha, na kuwaikilisha dini kwa sura ambayo sio yenyewe, hili ni jambo ambalo  Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya inaliepuka.

“Maisha ya binadamu ni roho na mwili; lazima apate mafunzo ya kupata maendeleo ya kimwili na wakati huo huo apate maendeleo ya kiroho, chochote ukikiacha kingine kinapoteza maana yake,” alisema Shekhe Abdurahman.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles