24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

STAMICO yaja na mkaa mbadala kulinda mazingira

Na Anna Ruhasha, Geita

Katika kulinda utunzaji wa mazingira nchini Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza kutengeneza mkaa mbadala wenye bei nafuu ili kusaidia wananchi kuachana na uharibifu wa mazingira hasa ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa.

Afisa masoko kutoka STAMICO, Mark Stephano akizungumza na Wenyeviti wa Halmashauri ya Geita waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya tano ya teknolojia ya madini yanayoendelea mjini Geita, amesema mkaa huo utakuwa rafiki wa mazingira.

Amesema STAMICO katika kuthamini na kujali wamekuja na mkakati huo ikiwa ni sehemu ya kujivunia miaka 50 ya utafiti na usimamizi wa madini nchini na kuendelea kuwasisitiza wadau wao kutunza mazingira.

“Mkaa huu utakuwa rafiki mkubwa wa mazingira kwa ni utaokoa ukataji miti ambayo imekuwa ikikatwa kwa ajili ya kuchoma mkaa, hivyo huu wetu ni gharama nafuu kwani unatokana pia na taka,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzao mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita, Constatine Mtani mbali na kuipongeza STAMICO pia ameomba wanachi kutumia maonyesho hayo kujifunza hasa katika kutengeneza mkaa huo ili kuondokana na ukataji wa miti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles