26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji Yanga wapewa siri kuiua Ahly

Azam-vs-Yanga-3NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amewapa majukumu wachezaji wa timu hiyo akiwataka kutulia na kujipanga upya kwa mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri baada ya kusoma mbinu za wapinzani wao walipokutana juzi.

Licha ya kupata matokeo ya sare ya bao 1-1 nyumbani, kocha huyo raia wa Uholanzi, amejipa matumaini ya kushinda ugenini na kusonga mbele katika michuano hiyo kwa kuwaondosha miamba hao wa soka barani Afrika.

Matokeo ya mchezo wa juzi wa hatua ya 16 bora uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wawakilishi hao wa Tanzania walijiweka kwenye wakati mgumu watakaporudiana ugenini Aprili 20, mwaka huu ambapo Yanga watahitaji ushindi au sare ya zaidi ya bao moja.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Pluijm alisema anaamini lolote linaweza kutokea lakini bado ni mapema sana kukata tamaa na kupoteza matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Pluijm aliyeiongoza Yanga kuziondosha nje ya michuano hiyo timu za Cercle de Joachim ya Mauritius na APR ya Rwanda katika hatua za awali, alisema mchezo wa marudiano utakuwa ni kibarua kizito kwao kuhakikisha wanafanya vyema na kuendeleza kasi yao.

“Hatuwezi kupoteza matumaini ya kuwafunga Al Ahly ugenini ingawa kwa uchezaji wao wa juzi tayari wameonyesha ni namna gani wamepania kutwaa ubingwa ambao unashikiliwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),” alisema.

Mholanzi huyo alisema matokeo waliyopata juzi yanahuzunisha lakini bado wanayo nafasi ya kufanya maandalizi ya muda mfupi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ambao wamepania kupambana ili kuifikisha mbali timu hiyo kimataifa.

Wakati huo huo, mashabiki wa Yanga walioshuhudia mchezo wa juzi walisifu kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji, Donald Ngoma, huku wakieleza kuwa fedha zilizotumika kumsajili nyota huyo wa Zimbabwe zilikwenda kihalali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles