27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yaizamisha Esperance

mtanzania jumatatu.inddTHERESIA GASPER NA MWALI IBRAHIM, DAR

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Azam FC jana waliutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Azam Complex baada ya kuisambaratisha timu ngumu ya Esperance ya Tunisia kwa kuichapa mabao 2-1.

Matokeo ya ushindi wa jana katika mchezo huo wa hatua ya 16 bora, yamewarahisishia kazi Azam watakaporudiana ugenini Aprili 20, mwaka huu na wapinzani wao katika Uwanja wa De Rades, uliopo jijini Rades, Tunisia.

Azam kwa upande wao wameanza vyema mchezo wa awali tofauti na wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Yanga waliolazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Katika mchezo wa jana, Esperance walioanza kwa kuisoma vizuri Azam, walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 33 kupitia kwa Haithem Jouin aliyeunganisha vyema krosi ya Ilyes Jelassi.

Timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza huku wenyeji Azam wakikosa nafasi nyingi za wazi zilizotokana na wachezaji kukosa umakini wanapofika langoni mwa wapinzani.

Kipindi cha kwanza kilimalizika huku Esperance wakiongoza kwa bao moja, jambo lililomfanya kocha wa Azam, Stewart Hall, kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kumtoa Michael Bolou na kumwingiza, Frank Domayo.

Mabadiliko hayo yalizaa matunda kwa Azam kwa kuongeza mashambulizi ambapo dakika ya 48 mshambuliaji, John Bocco, alishindwa kuunganisha vyema mpira wa krosi iliyochongwa na Erasto Nyoni baada ya shuti alilopiga kutoka nje la lango.

Azam walizidisha kasi ambapo dakika ya 68 kiungo, Farid Mussa alifanikiwa kusawazisha bao baada ya kuunganisha kwa shuti kali pasi ya Ramadhani Singano ‘Messi’.

Bao hilo lilifufua matumaini na kuongeza morali kwa wachezaji wa Azam ambao walifanikisha kupatikana bao la pili dakika ya 70 kupitia kwa Singano akiunganisha vyema krosi iliyochongwa na Farid.

Dakika ya 84 beki wa Azam, Pascal Wawa, aliumia vibaya na kushindwa kuendelea na mchezo ambapo nafasi yake ilichukuliwa na David Mwantika.

Azam: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum/Khamis Mcha, Agrey Morris, Pascal Wawa/David Mwantika, Jean Mugiraneza, Kipre Tchetche, Michael Bolou/ Frank Domayo, Ramadhani Singano ‘Messi’, John Bocco, Farid Musa.

Esperance: Moez Ben, Cherifia Iheb Mbaarki/Amine Nefzi, Yacine Rabii, Mohamed Ally, Chamseddine Dhaouadi, Hoiucine Ragued, Fausseny Coulibaly, Driss Mhirsi/Adem Rjaibi,  Ilyes Jelasii/Chaker Reguii, Fakhreddine Ben Youssef, Haithem Jouin.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles