25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WAASI SUDAN KUSINI WAPATANA KUMNG’OA RAIS KIIR

JUBA, SUDAN KUSINI


MAKUNDI ya upinzani akiwamo kiongozi wa waasi nchini hapa, Riek Machar, yamesema wamekubaliana kushirikiana kwa karibu ili kuingoa Serikali ya Rais, Salva Kiir.

Watia saini wa makubaliano hayo ni pamoja na mawaziri wa zamani wa serikali hiyo, Kosti Manibe na Lam Akol, pamoja na Thomas Cirillo Swaka, mkuu wa zamani wa jeshi wa masuala ya lojistiki, ambaye alijiuzulu Februari mwaka huu kwa kile alichokiita ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi huku likidhibitiwa na kabila la Dinka la Rais Kiir.

"Kwa kufanya kazi pamoja, juhudi zetu, kisiasa, kidiplomasia na kijeshi kutaleta ufanisi zaidi wakati tukijigawa katika vitengo tofauti," alisema Nathaniel Oyet, ofisa mwandamizi wa kundi la Machar la SPLA-IO.

Sudan Kusini ilipata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka 2011 lakini ikatumbukia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe miaka miwili baadaye baada ya Kiir kumtimua makamu wake  Machar anayetoka kabila la Nuer.

Hatua hiyo ilisababisha machafuko yaliyoegemea zaidi misingi ya kikabila na kuziingiza sehemu kubwa za taifa hili katika baa la njaa, na kulazimisha robo ya wakazi wa taifa hili kukimbia makazi yao.

Umoja wa Mataifa umesema machafuko yaelekea kuwa ya utakasishaji kabila na kuhatarisha kuwa ya kimbari.

Kund la Machar, SPLM-IO limepambana na askari watiifu kwa Kiir kwa zaidi ya miaka mitatu lakini majenerali wake kadhaa wamejitoa ili kuanzisha vuguvugu lao au kujiunga na serikali ya Kiir.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles