23.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

K/KASKAZINI: KOMBORA JIPYA LINA UWEZO WA KUBEBA NYUKLIA

SEOUL, KOREA KUSINI


MAMLAKA za Korea Kaskazini zimedai kombora jipya la masafa marefu lililofanyiwa majaribio siku ya Jumapili linauwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia .

Kombora hilo lililorushwa na kwenda angani kwa urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri umbali wa kilomita 700 kabla ya kuanguka baharini magharibi mwa Japan.

Korea Kaskazini ilisema siku ya Jumatatu ni jaribio la uwezo wa kombora jipya.

Jeshi la Korea Kusini limesema haliweza kuthibitisha madai hayo ya Korea Kaskazini.

Lakini limesema kuwa kombora hilo lilionekana kuweza kuruka angani, hatua ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa makombora ya masafa marefu, kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Yonhap.

Majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani.

Marekani na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo.

Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema kwamba jaribio la kombora jipya la masafa marefu la Hwasong 12 lilifanyika kama ilivyopangwa.

Limesema kuwa jaribio hilo lililenga kuonyesha kwamba kombora hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa cha Nyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,293FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles