24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi 26 washinikiza mkurugenzi wa Sauti ya Amerika ajiuzulu

Washington, Marekani

Waandishi wa habari 26 wanashinikiza mkurugenzi wa Sauti ya Amerika ajiuzulu.

Hatua hii ni baada ya mtiririko wa madai ya hatua za ulipizaji kisasi na ukiukaji wa sheria ambazo zimewekwa kulinda uhuru wa waandishi ziliyopelekea kupewa majukumu mengine mmoja wa waandishi waandamizi wa Sauti ya Amerika, VOA.

Taarifa iliyosambazwa Alhamisi inamshutumu mkurugenzi Robert Reilly na naibu mkurugenzi wake, Elizabeth Robbins, kwa kuvunja muongozo unaofuatwa na waandishi wa habari wa VOA kwa kumwezesha Afisa wa ngazi ya juu wa serikali “fursa ya kuwa huru kuzungumza mubashara katika matangazo ya kitu hicho” kwa kuandaa matangazo ya moja kwa moja ya Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo na baadae kumuondoa mwandishi wa habari wa VOA White House baada ya kujaribu kumhoji waziri anaye maliza muda wake.

Mradi wa Kuiwajibisha Serikali (GAP), usiokuwa wa faida unaowatetea wanaotoa taarifa, umeufahamisha uongozi wa Shirika mama la Vyombo vya Habari vya Umma Marekani, USAGM na VOA, pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Maalum, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu, Kamati ya Masuala ya Mambo ya Nje na wabunge wengine, kuwa wale waliosaini malalamiko hayo wanachukuliwa kuwa ni watoa taarifa wanaolindwa.

Patsy Widakuswara, aliyejiunga na VOA mwaka 2003, aliambiwa jioni Jumatatu kuwa anapangiwa majukumu mengine, saa kadhaa baada ya mwandishi huyu maarufu alipojaribu kumuuliza Pompeo na baadae Reilly wakati waziri alipokuwa akiondoka katika jengo la makao makuu ya VOA.

Katika hotuba yake, waziri wa mambo ya nje anayemaliza muda wake alimpongeza Michael Pack, mtendaji mkuu, kwa mabadiliko aliyoyatekeleza USAGM chini ya uongozi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles