Matokeo rasmi ya uchaguzi Uganda kutangazwa jioni

0
489

Kampala, Uganda

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda inaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Januari 14, huku matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais yakitarajiwa kutolewa leo jioni.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Rais aliyeko madarakani, Yoweri Museveni anayewania nafasi hiyo kwa muhula wa sita kupitia Chama tawala cha NRM anaongoza kwa asilimia 61.98, ambazo ni sawa na kura 4,340,134.

Mpinzani wake Mkuu, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha NUP amepata asilimia 30.91 sawa na kura 2,164,347.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na mgombea wa chama cha Forum for Democratic Change, FDC, Amuriut Oboi Patrick ambaye kapata asilimia 3.64, ambazo ni sawa na kura 254,628 ya kura zilizohesabiwa.

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda inaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Januari 14, huku matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais yakitarajiwa kutolewa Jumamosi jioni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here