28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Umoja wa Mataifa wamuidhinisha mpatanishi mpya wa Libya

New York,Marekani

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha uteuzi wa mwanadiplomasia Jan Kubis kuwa mjumbe mpya wa Libya wa umoja huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alipendekeza Kubis achukue nafasi ya Ghassan Salame ambaye alijiuzulu Machi mwaka uliopita kwa sababu za kiafya.

Stephanie Williams, ambaye ni msaidizi wa Salame, amekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda. Kubis, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Slovakia, kwa sasa ni mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon.

Amewahi pia kuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Afghanistan na Iraq. Uteuzi wa Kubis, unafanyika baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Desemba kuidhinisha mpango wa Guterres kumteua mwanadiplomasia wa Bulgaria, Nickolay Mladenov kushika nafasi hiyo.

Lakini wiki moja baadae Mladenov alisema hawezi kuwa mjumbe wa Libya kwa sababu binafsi na za kifamilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles