26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Guterres aonya ubinafsi kwenye chanjo ya corona

New York, Marekani

Historia ya kuvunja moyo imefikiwa duniani ambapo watu milioni 2 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa utokanao na virusi vya Corona au COVID-19, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres jana.

Kupitia ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video, Guterres amesema nyuma ya takwimu hizo ni majina ya watu na nyuso zao. 

“Tabasamu zao zimesalia historia, viti walivyokuwa wanaketi wakati wa mlo wa usiku sasa ni vitupu, na vyumba sasa vimebakia na mwangwi wa ukimya wa wapendwa wetu,” amesema Guterres.

Katibu Mkuu amesema cha kusikitisha zaidi, madhara ya janga la Corona yamekuwa mabaya zaidi kutokana na ukosefu wa juhudi za pamoja za kimataifa.

Ni kwa mantiki hiyo amesema katika kukumbuka watu hao milioni 2 waliopoteza maisha kutokana na Corona, dunia inapaswa kuchukua hatua kubwa zaidi za pamoja na kwa mshikamano.

Hivi sasa chanjo salama na fanisi dhidi ya  Covid-19 zinaanza kusambazwa, na Umoja wa Mataifa unasaidia nchi kuhamasisha hatua ya kihistoria ya kimataifa ya utoaji chanjo.

“Lazima tuazimie kuhakikisha kuwa chanjo hizo zinaonekana kuwa jambo jema kwa umma wa kimataifa, chanjo za watu. Hii inahitajia ufadhili kamilifu wa kufanikisha mpango wa pamoja wa kuhamasisha na kusambaza chanjo dhidi ya Corona, au COVAX ambao umejipambanua kuhakikisha kuwa chanjo zinaweza kupatiwa kila mtu,”  amesema Guterres.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles