21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mfahamu HI-DEF, rapa mwenye mipango ya kutikisa dunia

Seattle WA, Marekani

Muziki wa Hip hop umeendelea kushuhudia ongezeko la rapa wanaokuja na changamoto mpya zinazokuza utamaduni huo wenye mamilioni ya wafuasi ulimwenguni kote.

Kutoka Seattle Washington nchini Marekani, kutana na Henry Samuel Dubar maarufu kama HI-DEF, rapa mwenye mipango ya kutikisa dunia kupitia muziki wa Hip hop.

HI-DEF ni nani?

Anasema yeye ni kijana mpambanaji anayefanya utamaduni wa Hip hop kupitia nguzo zake za muziki, graphics design na Cinematography huku akiwa ni mwanamitindo huru aliyezaliwa miaka kadhaa iliyopita huko Lansing, Michigan na kukulia kwenye familia yenye asili ya Liberia.

ALIVYOINGIA KWENYE MUZIKI

Dubar alianza kuonyesha kipaji chake kwa kufanya aina mbalimbali za muziki akiwa na umri mdogo kuanzia shuleni (high school) mpaka chuo ambapo jamii yote inayomzunguka ilikuwa haina shaka juu ya talanta kubwa aliyokuwa nayo.

Akiwa kwenye harakati zake za muziki, mwaka 2014 alitengeneza na kuachia kanda mseto (mix tape) ya kwanza iliyoitwa SESSIONS II na akafanikiwa kuuza nakala 500 kwa kutembeza kwenye gari lake.

AENDELEA KUFANYA MAAJABU

Mwaka mmoja mbele aliachia albamu yake ya kwanza inayoitwa OTL ambayo ilifanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali ya kusikiliza na kununua muziki.

Ilipofika 2020 rapa HI-DEF aliachia albamu yake ya nne iliyoitwa WORLDWIDE ikiwa imetengenezwa na prodyuza Keyboard Kid na akawashirikisha wasanii kibao akiwamo Project Pat.

Rapa huyo ambaye amekuwa karibu zaidi na jamii yake, tangu mwaka 2010 alipoanza kupata umaarufu ameendelea kutoka audio na video kali zenye maudhui mbalimbali yanayo onya, kosoa jamii na kuacha burudani kwa wapenzi wa Hip hop.

Aidha HI-DEF, amefahamika kwa kutengeneza majina mbalimbali yanayotumika kwenye jamii yake kama vile Black Milk, Nappy Roots, Futuristic, Ugly God, Obie Trice, Curren$y na Masta Ace.

Ameendelea kutamba kwamba yeye ni kioo kwa kizazi kipya cha Hip hop (new school), kwa sababu jamii imemuelewa na ana mipango mingi inayotekelezeka ya kutikisa dunia kupitia sanaa siku za mbeleni.

Katika kudhihirisha hilo, ngoma za HI-DEF zilizopo kwenye mradi wake wa Megastar Buzzing (Strong Feelings) imeanza kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya redio kama vile Spoon 107.5, redio ambayo hucheza nyimbo za wasanii daraja la kwanza duniani ( A list artists).

“Haya ni mafanikio makubwa kwangu na jamii nzima hasa wafuasi wa Hip hop, nakaribisha maoni na ushauri juu ya sanaa yangu kupitia kurasa zangu za Instagram, Facebook na Twitter natumia jina HI-DEF,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles