25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Vurugu Afrika Kusini; Zambia yasitisha mechi na Bafana Bafana

ABASI SHABANI (UDSM-SJMC)

Shirikiso la Mpira wa Miguu nchini Zambia (FAZ), limeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika Kusini (SAFA) ikiiarifu lengo la kusitisha mechi ya kimataifa ya kirafiki baina yao na Timu ya Bafana Bafana iliyotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii katika dimba la National Heroes, jijini Lusaka, Zambia kutokana na hali ya machafuko yanayoendelea nchini humo.

Ujumbe huo uliosomeka: “Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), tunaomba radhi kuwataarifu wenzetu (SAFA) kuwa mechi iliyotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili katika Uwanja wa National Heroes imeahirishwa kutokana na hali ya kiusalama kwa ndugu zetu nchini Afrika Kusini”.

Kutokana na taarifa hiyo ya kusitishwa kwa mechi na Zambia Wanachipolopolo, shirikisho lenye dhamana wa mpira wa miguu nchini Afrika Kusini (SAFA) imeanza mchakato wa kusaka timu nyingine ya kucheza nayo kutokea ukanda wa COSAFA ambayo inautayari.

SAFA kupitia Ofisa Habari wake, amekiri kupokea barua hiyo, ambapo amesema iliyochukuliwa na ZAF, na kusema mechi hiyo imeahirishwa.
“Tumepokea taarifa kutoka kwa wenzetu SAFA kuwa hawatacheza mchezo dhidi yetu kufuatia machafuko yanayoendelea hapa nyumbani, ikiwemo kupigwa kwa ndugu zao wa Zambia wanaoishi nchini humu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles