24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: nimewasamehe January, Ngeleja kwa kunitukana

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amesema amewasamehe Mbunge wa Bumbuli, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kwa kumtukana kwenye simu.

Rais Magufuli amesema hayo leo katika mkutano wa wahandisi na wadau wa sekta ya ujenzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 4.

“Nakumbuka hivi karibuni kuna watu walinitukana na nikapata uhakika kwamba sauti zile ni zao, nikafikiria nikasema hawa wakipelekwa kwenye kamati ya siasa adhabu itakuwa kubwa. Walinitukana kwenye simu na nikahakikisha ni kweli ni sauti zao lakini nimewasmaehe

“Lakini wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha nikasema nisipowasamehe nitabaki na maumivu makubwa sana watu hao ni January Makamba na Wiliam Ngeleja nikaona niwasamehe tu.

“Waliomba msamaha nikasema ni vijana ni na nimewasamehe. Kama palikuwa na mambo mambo mabaya nyuma tuyasahau ili tukaanze upya maana kusamehe siyo jambo rahisi lakini saa nyingine inabidi usamehe,,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles