27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Vitambulisho vya Mzanzibari vyazua balaa Pemba

Na Mwandishi Wetu, Pemba
HALI ya siasa visiwani Zanzibar imeanza kuwa tete baada ya wabunge na wawakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF), kuwaongoza wananchi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba waweze kupewa vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya tangazo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hemed Suleiman Abdallah la kuwataka wabunge na wawakilishi kwenda kuwahamasisha wananchi wakachukue vitambulisho vyao.
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohamed Habib Mnyaa na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haji Faki Shaali, ambaye pia ni Mwakilishi wa Mkanyageni (CUF) ilibidi waingilie kati.
Akizungumza na waandishi wa habari huku akiwa na wananchi wapatao zaidi ya 800 waliojitokeza kwenda kuchukua vitambulisho vyao, alisema anasikitishwa na hatua ya Ofisa Vitambulisho wa Pemba, Omari Ngwali kuwa na lugha za kupishana katika utoaji wa vitambulisho hivyo.
Alisema ofisa huyo amekuwa akiwaambia watu wakachukue vitambulisho vyao kila Jumatatu aamekuwa akishindwa kufika ofisini kwa mujibu wa utaratibu.
“Tumefika hapa nikiwa na wenzangu, tukampigia simu akasema vitambulisho havipo lakini kuna ofisa wao ametumwa Unguja yuko kwenye meli itafika leo (jana), jioni. Lakini ni uongo kwani kwa mujibu wa ratiba hakuna meli inayokuja leo Pemba.
“Nilikuwa mimi, Mbunge wa Mkoani Ali Khamis Seif, Waziri asiye na Wizara Maalum Haji, Haji Faki Shaali, Mwakilishi wa Mtambile Mohamed Haji Kingunde, Mwakilishi wa Chambani Mohamed Mbwana, Katibu wa CUF Wilaya ya Mkoani Saidi Aweso pamoja na Mkurugenzi Abas Juma Muhunzi,
“Pamoja na kumpa taarifa zote lakini DC hakuamini taarifa hizo akasema hana habari za avitambulisho hivyo. Je, haki iko wapi kwa wananchi? Tumetoka mashambani kuja kuchukua vitambulisho vyetu na hakuna shughuli iliyofanyika,” alisema Mnyaa.
Alipotafutwa na mwandishi kwa simu kutoka Dar es Salaam jana, Ofisa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi, Omari Ngwali, alisema anaomba apewe muda aweze kuzungumza.
“Mimi sikujui kwanza kama wewe ni mwandishi nataka nikufahamu, nipe dakika moja nipo katika sehemu mbaya kidogo,” alisema na kukata simu.
Hata hivyo, alipotafutwa baada ya muda, simu yake iliita bila kupokewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles