29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kada CCM ampiga katibu wake

NA ELIYA MBONEA, SIMANJIRO
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Kata ya Endiamtu Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Issa Katuga anadaiwa kumpiga ngumi na mateke Katibu wa chama hicho, Salimu Kombo baada ya kumtuhumu kugoma kuidhinisha matumizi ya Sh bilioni moja kwa ajili ya kwenda kulipa madeni.
Tukio hilo linadaiwa kutokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ofisi za CCM za kata hiyo, baada ya Mwenyekiti Katunga kumtuhumu katibu wake kuwa amegoma kuidhinisha fedha hizo za madeni.
Tukio hilo ambalo lilivuta hisia za wananchi, lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, ambaye alisema bado wanaendelea na upelelezi.
Akizungumzia tukio hilo, Kombo alisema mwenyekiti wake alimpiga hadi akapoteza fahamu.
“Hizi fedha zimetokana na mnara wa Kampuni ya Airtel ana mwenyekiti alitaka zitolewe ndipo wajumbe wakagoma kuidhinisha. Baada ya hapo aliniita ofisini jioni na kuniuliza kwa nini niligoma.
“Tukiwa ofisini ndipo alianza kunipiga ngumi kichwani, usoni, puani na mdomoni na kusababisha nipoteza fahamu na baada ya kuzinduka nilijikuta sina fedha Sh 100,000 na simu ya mkononi aina ya Tecno.
“Baada ya hapo nilikwenda moja kwa moja kituo cha pilisi kisha nikapewa maelekezo ya kwenda Kituo cha Afya Mirerani kwa ajili ya matibabu,” alidai Kombo.
Akijibu tuhuma hizo, Mwenyekiti Katunga, alikana kumshambulia kiongozi huyo ingawa wamekuwa na tofauti za mtazamo katika uongozi wao.
“Sijafanya kitendo kama hicho ingawa tuna mitazamo tofauti ya uongozi. Mara nyingi tunapingana kwenye vikao siwezi kumpiga nadhani maadui wangu wa siasa wamemchochea anituhumu,” alisema Katuga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles