29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bilal aongoza waombeleza msiba wa John Nyerere

johnNa Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam
MAKAMU wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal jana aliongoza mamia ya waombolezaji wakiwamo viongozi wa vyama na Serikali kuaga mwili wa mtoto wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, John Nyerere.
Mbali na Dk. Bilal viongozi wengine waliokuwapo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete.
Akisoma wasifu wa marehemu, mdogo wake, Makongoro Nyerere alisema alizaliwa Mei mwaka 1957 katika Kijiji cha Komuge Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Alisema alianza elimu ya msingi mwaka 1964 katika shule ya msingi Arusha na baadaye kuhamia shule ya Mtakatifu Joseph Dar es Salaam.
Mwaka 1972 alijiunga na shule ya Sekondari Tambaza Dar es Salaam na mwaka 1975 alimaliza elimu yake katika sekondari ya Mazengo Dodoma.
Mwaka 1974 alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na alipokuwa jeshini aliweza kuhudhuria kozi mbalimbali ikiwamo ya urubani wa ndege za vita na kuhitimu mwaka 1977 nchini China.
Baada ya kumaliza kozi hiyo alipangiwa katika kikosi cha Ngerengere na alistaafu jeshini kwa hiari mwaka 1979.
Alisema baada ya hapo alikua akijishughulisha na kilimo na ilipofika mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sarion, Korea.
“Marehemu aliugua maradhi ya muda mrefu na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),” alisema Makongoro.

Alisema alifariki dunia Mei 9 mwaka huu baada ya juhudi za kumpatia matibabu kushindikana.
“Tunalishukuru sana JWTZ kwa kushirikiana na sisi tangu Mwalimu akiwa hai hadi alipofariki dunia ndiyo maana wamejitolea kutusaidia mambo mbalimbali yanayojitokeza katika familia yetu,” alisema Mkongoro.
Mdogo huyo wa marehemu baada ya kutoa maelezo hayo aliangua kilio hali iliyowafanya waombolezaji kumsaidia kumweka pembeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles