23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Virusi vipya vya corona: Uingereza yarejesha hospitali za dharura

London, Uingereza

Kituo kinachotoa taarifa za COVID-19 cha Johns Hopkins kimeripoti mapema Jumamosi kuwa kuna zaidi ya watu milioni 84 duniani wenye maambukizi ya virusi vya corona.

Marekani inaendelea kuwa na maambukizi zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ambapo kuna zaidi ya maambukizi milioni 20, takriban robo ya maambukizi yote duniani.

India ina idadi ya juu ikiwa ya pili kwa maambukizi ambapo kuna zaidi ya milioni 10, ikifuatiwa na Brazil ikiwa na maambukizi milioni 7.7.

Maafisa wa afya wa Uingereza wameanza tena kutumia hospitali za dharura ambazo zilijengwa wakati janga lilipoanza huku nchi hiyo ikipambana kukabiliana na kusambaa kwa maambukizi zaidi ya aina mpya ya virusi vya corona.

Msemaji wa Huduma ya Taifa za Afya Uingereza amesema wafanyakazi wa afya wanajiandaa kufungua tena hospitali za Nightingale za London iwapo ikutakuwa na haja ya kufanya hivyo, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Hospitali za muda za Nightingale ziliwekwa na jeshi katika maeneo mbalimbali kuzunguka mji huo na ziliendelea kuwa tayari baada ya kutumika kidogo wakati wa wimbi la kwanza la maambukizi ya virusi vya corona.

Siku ya Ijumaa, Uingereza ilirekodi maambukizi mapya 53,285 ya COVID-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona.

Idadi hiyo ni ya chini kidogo ikilinganishwa na ile ya rekodi ya nyuma ya maambukizi 55, 892, lakini ni siku ya nne leo mfululizo kwamba maambukizi mapya yamevuka 50,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles