24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, October 24, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa umma kuchunguzwa

Samia Suluhu HassanNa Mwandishi Wetu

-MTWARA

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuchunguza na kuwachukulia hatua za kisheria na za kinidhamu, viongozi na watumishi wa umma wanaokiuka taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa, wakati anafungua jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu takribani Sh bilioni mbili.

Alisema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma, hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji kazi miongoni mwa watendaji hao.

“Serikali itaendelea kuiimarisha Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi,” alisema Samia

Alisema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia myenendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawajaleta madhara kwa Serikali na jamii kwa ujumla.

Alitoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi hiyo kwa kutoa taarifa kuhusu myenendo ya viongozi wanaokiuka maadili ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Katibu wa Sekreterieti hiyo, Jaji Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo aliiomba Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kwa nchi nzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles